The Church is ONE
The Church is HOLY
The Church is CATHOLIC
The Church is APOSTOLIC!
Viva Cristo Rey!
Kristo sharti atawale!
Alexander retweeted
Kuna kipindi cha maisha kinaitwa Pruning Season.
Ni pale Mungu anaanza kukuondolea vitu ulivyovipenda.
Marafiki wanaondoka.
Maisha yanakuwa ya ukimya.
Unaweza ukafikiri umepoteza watu.
Kumbe unaandaliwa kubeba vitu ambavyo usingeweza kubeba ukiwa kwenye kelele nyingi.
Ee Bwana uliye waambia Mitume wako, Amani nawaachieni, amani yangu nawapa. Usizitazame dhambi zetu ila tu imani ya Kanisa lako. Upende kulijalia amani na umoja kama yalivyo mapenzi yako. Unayeishi na kutawala daima na milele, Amina🙏
Alexander retweeted
Warumi 12:12 ↩️
Kwa tumaini mkifurahi; katika dhiki mkisubiri; katika kusali mkidumu.
Tukumbuke kuanza na Mungu kwanza 🙏🏽
Alexander retweeted
A 27-year-old priest knew he was going to die. Three months before he died, he told a fellow priest about it. Calmly, with clarity, not as a guess but as a fact he had accepted. His name was Miroslav.
THE CALLING
He was born in 1920 in a small village in Istria, Croatia. Young and called to serve, he studied in Rome to become a priest. When World War II broke out, he was recalled home and ordained in 1943, in the middle of the war. He became something rare, a priest people actually loved. He brought his parishes alive. He filled them with the sacraments, with faith, with hope. He was fearless and he was gifted. He was just getting started. Then the war ended and a new enemy took control.
THE PRESSURE
Communist Yugoslavia took power in 1945. Their mission was clear: crush the Church, erase it, control it and make it disappear. Bishops were arrested, priests were harassed, beaten and imprisoned. The great Archbishop of Zagreb was thrown into prison. The message was unmistakable, bend to the state, or be destroyed. Most priests learned to stay quiet. It was the only way to survive, Miroslav would not.
THE DEFIANCE
He spoke out, he defended his faith openly. He protected younger priests from persecution. He stood between the state and the people they wanted to break. That made him visible, that made him dangerous. By summer 1947, as he watched the regime tighten its grip, as he saw the danger closing in, something shifted in him. He wasn't afraid. He was ready. He told his seminarians: “Being a priest means being willing to shed your blood for the faith.” In June, he wrote in his diary to God: “If it is Your will, I wish to come to You as soon as possible.” He knew, and he was at peace.
THE MOMENT
On August 24 1947, he travelled to a small village called Lanisce. His mission was simple. Beautiful, the kind of thing priests have done for centuries: confirm children in the faith. Lay hands on young believers and strengthen them as Catholics. Give them the sacraments the regime wanted stamped out. He did it anyway.
In the open and unafraid. After the Mass, he and another priest went to the parish house to confirm those who had arrived late. It was around 11 am in the morning, then the door burst open. A group of Communist supporters stormed in. They seized him. They threw him to the ground and pinned him down. They stabbed him again and again, in the neck. His blood ran across the floor and up the walls. As his life left him, Miroslav cried out twice: “Jesus, take my soul.” Then he was gone.
THE SILENCE
The regime tried to erase him. His family wanted to bury him in his home village and they refused. They made his grave a thing to control, a symbol of their power. For decades, his story survived only in whispers in his own corner of Croatia, among people who loved him and refused to forget. The rest of the world never knew his name.
THE RESURRECTION
Then communism fell and in 2013, 66 years after his death, the truth could finally be told. The Catholic Church declared Miroslav Bulesic a martyr. Blessed, honoured at last.
The ceremony took place in Pula, in an ancient Roman arena built two thousand years before. Twenty thousand people gathered in that amphitheater to say, this man's name will not be forgotten. His blood was not spilled in vain. The men who killed him wanted him erased forever. Instead, his name is now spoken in churches around the world. He could have stayed quiet, played it safe and survived. Instead, he chose to be faithful, to protect others and to stand for something larger than himself. Even knowing the knife was coming.
His crime? Confirming children in their faith. His legacy? A young man who saw his own death approaching and did not blink. Who prayed even as he died.
Whose last breath was a prayer, not a scream. “Jesus, take my soul.” They tried to bury him twice. Once in the ground and once in silence, he rose above both.
NOVENA YA KRISTO MFALME
SIKU YA 05
*Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.*
TAFAKARI
"Ufalme wa Neema"
“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, amejaa neema na kweli; tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba. Na katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, neema juu ya neema” (Yoh 1:14, 16).
“Basi tukitenda kazi pamoja naye, twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure” (2 Kor 6:1).
Bwana Yesu Kristo, Mfalme wa milele na wa ulimwengu wote, ambaye kwa neema yako tunazaliwa upya kama wana wa Mungu, usituache tufanane na ulimwengu huu wenye utamaduni wa kifo.
Utugeuze kwa kuzifanya upya nia zetu, ili tufikiri na kutenda bila kutumainia itikadi za zama zetu, tusitegemee nguvu za kidunia, tusitafute utukufu wa ulimwengu huu, bali kwa nuru na nguvu ya neema yako; kwa utukufu wa Ufalme huo, ambapo unaishi na kutawala pamoja na Baba, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele,Amina.
Mungu Mwenyezi wa milele, umefanya upya viumbe vyote katika Mwanao mpendwa, Mfalme wa ulimwengu wote. Watu wote wa dunia, ambao sasa wamejeruhiwa kwa jeraha la dhambi, wawe chini ya utawala wa upole wa Mwana wako wa pekee. Anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja milele na milele.
Kristo, Mwokozi wetu na Mfalme wetu, fanya upya ndani yetu ujasiri wa kuwa waaminifu kwa Ufalme wako. Tunaomba neema ya kukuweka wewe juu ya mambo yote ulimwengu huu.
Ewe Mfalme wa Amani, ufalme wako ufike katika maisha yetu na katika maisha ya dunia nzima. Kristo Mfalme wetu, kwa huruma yako tunaomba ujibu maombi yetu kama yanapatana na Mapenzi yako Matakatifu…*[Taja nia yako hapa]*
Tunapotafakari ujio Wako wa pili na hukumu ya wanadamu wote, tunakusihi uturehemu na utupe neema ya kuwa Watakatifu. Tunaomba kwamba sio tu tukae nawe bali pia ututumie sisi wenye dhambi kuwaleta wengine katika Ufalme wako.
Kristo Mfalme, Ufalme wako ufike!
Amina.
LITANIA YA KRISTO MFALME
Bwana, utuhurumie
Kristo, utuhurumie
Bwana, utuhurumie.
Baba wa Mbinguni Mungu, Utuhurumie.
Mwana Mkombozi wa dunia Yesu, Kuhani wetu Mkuu, Nabii wa Kweli, na Mfalme wetu Mkuu, Utuhurumie.
Roho Mtakatifu Mungu, Utuhurumie.
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja, Utuhurumie.
Kristo Mfalme, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme mwingi wa rehema, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye kwa Rehema yako Kuu tumepewa Sakramenti ya Kitubio, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme wa Upendo ambaye hutupatia Neema yako ya uponyaji, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme katika Ekaristi, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme uliyetabiriwa na manabii, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme wa Mbingu na dunia, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme na Mtawala wa Mataifa Yote, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme furaha ya Mbinguni, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme mwenye huruma kwa raia wako, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme uliyepewa mamlaka yote na Baba wa Mbinguni, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye kupitia kwako sisi tumefanyika kuwa wana wa Mungu, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye Ufalme wako sio wa ulimwengu huu, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye Moyo Wako Mtakatifu umejaa Upendo kwa wanadamu wote, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye ni Mwanzo na Mwisho, Alfa na Omega, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme ambaye ametupa Maria Malkia, kuwa Mama yetu pia, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye utakuja tena kwa Nguvu na Utukufu Mkuu, Tawala mioyo yettu.
Kristo Mfalme ambaye Enzi yako tunaikaribia kwa ujasiri, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme uliyepo kweli katika Sakramenti Takatifu, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye ulimfanya Maria kuwa Mgawaji wa Neema Zote, Tawala mioyo yetu.👇
1
18
423
Kristo Mfalme Ambaye ulimfanya Maria ashiriki katika Mpango wa Wokovu, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme unayeponya mgawanyiko na mafarakano yote, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme uliyejeruhiwa na kutokujali kwa wanadamu, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye unaweza kuufariji Mioyo iliyojeruhiwa, Tawala mioyo yetu.
Kristo Mfalme ambaye ndiye Chemchemi ya Furaha yetu, Tawala mioyoni mwetu.
Kristo Mfalme Mtawala wa nguvu zote za kidunia, Ufalme wako ufike
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, tiisha chini ya miguu yako nguvu za kuzimu, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Nuru ya nuru yote, angaza giza linalotuzunguka, Ufalme wako ufike
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Ambaye Rehema zako ni Kubwa sana hata kutupunguzia adhabu ambazo tunastahili kwasababu ya dhambi zetu, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa yote, uliyetambuliwa na kuheshimiwa na Mamajusi kama Mfalme wa Kweli, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Dawa Pekee ya ulimwengu huu geugeu, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Ambaye hubariki roho na mataifa ambayo yanakukubali kama Mfalme wao wa kweli, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Ambaye kwa huruma hututumia Malaika wako Watakatifu kutulinda, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, ambaye Jemedari wa ufalme wako ni Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, unayetufundisha kwamba kutawala ni kutumikia, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, hakimu wa Haki ambaye atawatenganisha waovu na wema, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, ambaye kila goti litapigwa, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Ambaye Utawala Wako ni Utawala wa milele yote Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, unayetuchunga kwa fimbo ya chuma, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa yote, haribu kila mamlaka na enzi ya mwovu shetani, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, ambaye Utawala wako hauna mwisho, Ufalme wako ufike.
Kristo Mfalme wa Mataifa Yote, Ambaye fadhili zako kwetu ni thabiti, na uaminifu wako wadumu milele, Ufalme wako ufike.
Baba wa Milele, Ambaye umetupa Mwana wako wa Pekee kuwa Mkombozi wetu, Mpatanishi wa Kweli na Mfalme wetu Mkuu, Tunakusifu na kukushukuru. Tunampenda Yesu, Mfalme Mkuu, aliyejishusha kwa Upendo kwetu na kuchukua hali ya mtumishi, Tunakusifu na kukushukuru.
Roho Mtakatifu, Upendo wa Baba na Mwana, unayetutakasa na kutupa Uzima, Tunakusifu na kukushukuru.
Maria Malkia na Mama yetu, ambaye unatupatanisha na Yesu kwa maombezi yako yasiyo na mwisho, utuombee.
Maria Malkia na Mama yetu, ambaye kupitia kwako Neema nyingi zinatujia sisi, Utuombee.
Maria Malkia na Mama yetu, kiashiria cha umoja wa Utatu Mtakatifu, Tunakupenda.
Malaika na Watakatifu wote wa Kristo Mfalme wetu, mtuombee na mtulinde.
KRISTO MFALME - UFALME WAKO UFIKE
KRISTO MFALME - UFALME WAKO UFIKE
KRISTO MFALME - UFALME WAKO UFIKE
Amina.
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
2
49
Siku moja utagundua kwamba baadhi ya mambo uliyokuwa unayahangaikia sana hata hayakuwa na thamani kubwa kama ulivyodhani. Bahati mbaya mida huo utakuwa huwezi kurekebisha tena ulipokosea. Linda amani yako, thamini afya yako, penda watu wako wa karibu. Hayo ndio ya muhimu zaidi.
Usiwe mtu ambaye watu wanamshukuru Mungu anapoondoka mahali iwe kazini, nyumbani, kwenye taasisi nk. Kuwa mtu ambaye uwepo wake unaleta amani, faraja na matumaini. Maisha ni mafupi sana kutumia nafasi yetu duniani kuongeza maumivu kwa watu wenaokuzunguka!
Usimtafute Mungu wakati wa shida pekee. Mungu si kituo cha dharura unachokikumbuka pale mambo yanapoharibika. Jenga uhusiano naye hata katika siku ambazo kila kitu kinaonekana kwenda vizuri.
Kuna tofauti kati ya kuijua Biblia na kuishi ujumbe wa Biblia. Unaweza kukariri maandiko mengi lakini ukashindwa kumsamehe aliyekukosea. Unaweza kuzungumzia upendo wa Mungu lakini ukakosa huruma kwa maskini. Imani inapaswa kuonekana katika matendo.
Alexander retweeted
The Holy Rosary is a beautiful gift that draws our hearts closer to Jesus through the intercession of His Blessed Mother.
If you believe in the power of rosary, type Amen.
ROZARI TAKATIFU - MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
1. Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
2. Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
3. Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
4. Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
5. Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
Usipime thamani ya maisha yako kwa kile ambacho bado hujakipata. Kuna mengi uliyonayo leo ambayo wenzako wanayatamani. Shukrani haimaanishi kwamba huna ndoto kubwa. Shukrani inamaanisha unathamini ulichonacho wakati unaendelea na safari ya kuelekea unakotaka kufika.
Hatari ya ujinga si kutokujua, bali ni kuamini kwamba unajua kila kitu. Mtu anayefahamu mipaka ya maarifa yake bado ana nafasi ya kujifunza. Mtu anayejiona ameshafika mwisho wa maarifa amejifungia milango ya hekima. Falsafa huanza kwa swali, si kwa kujifanya kuwa na majibu yote.














