Kwa umri wangu huu nitulie tuu na familia yangu yaa mwanamke nimemtongoza jana tuu leo anaomba pesa ili aende Mlimani City, mbaya zaidi kwa kumjaribu nikamwambia nitakupa 50k anasema haitoshi (mattercore yake)😂
Serikali iingilie kati hizi simu za mkopo ni zaidi ya kausha damu how come mtu simu ya 200k auziwe 800k?
Ameomba 10k nimemtumia muda huohuo unajua nini kimetokea 🤣🤣 eti mwanaume mbahili kama mpare yaani umeshundwa kutuma na ya kutolea? 😳 nimeumia saana mpaka Sasa nimerudisha muamala anauliza kwanini umesitisha muamala nimemjibu nikipata ya kutolea nitakumia tena🏃♂️🤣
Miradi mikubwa ya UJENZI ya serikali wanapewa makampuni ya kigeni lakini naona wanaojenga au watenda kazi ni wazawa wageni wao ni wasimamizi tuu Sasa kwanini tenda zisibaki kwa wazawa ili pesa ibaki hapahapa nyumani? Sijui nilitaka kusemaje🏃♂️
Malezi ya hiki kizazi ni hatari saana watoto hawana nidhamu imagine mtoto anaitwa na mzazi anaitikia WOOOZA.🤣
Boda kapigiwa simu na mteja ambaye ni mwanaume ili akamchukue mwanamke Lodge ampeleke nyumbani kwake jamaa kachukua boda ya rafiki yake maana yake ni mbovu kufika pale Lodge kumbe mwanamke mwenyewe ni mke wa boda you know what? Hayazungumziki🤫
Mke wa mtu kanifuata hapa anaomba tuzae mtoto 😳 kwakweli imenishitua saana, kuuliza sababu ya ombi lake aisee ni hatari saana kosa ni mme wake amezaa mtoto na mwanamke wa nnje na huyo mwanamke kamleta mtoto wa miezi 4 kwa baba yake na kumtelekeza hivyo mke anata kulipa kisasi.
Yaani naoa mke anatoka kwao na begi tuu anakuta kila kitu kipo nyumba, magari na mali zingine ila kwenye kuachana tugawane 50/50 hii sheria ilitungwa na nani?









