Paul Bonaventure (@Phbhimself) header
Paul Bonaventure (@Phbhimself) profile picture

|| PEACE MAKER ✌🏿 || Author | A human. Being. | Meditation & Energy-Based Teacher 🧘‍♀️| HipHop🎶 |

Somewhere in Africa
Joined January 2015
Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)Photo by Paul Bonaventure (@Phbhimself)
Watu wengi wamekuwa wakijifunza meditation tangu karne na karne, miaka na miaka. Sio kitendo kilichoanza hivi sasa bali ni kitendo kilichoanza tangu zamani na kimekuwa na faida mbalimbali kwa watu waliojifunza na kufanya taamuli. Wengine ni kutokana na kupunguza stress, kujifunza kuongoza akili zao, kuachana na mazoea wanayoshindwa kuyaacha na kutokana na kuongeza hekima ya kiimani. Ningependa kuelezea faida chache nzuri ambazo zinapatikana pale mtu anapofanya taamuli vyema na kwa mara kwa mara. • Taamuli (Meditation) inasaidia kutengeneza furaha ya ndani. Tunaposema furaha ya ndani tunamaanisha nini? Ni furaha unayotembea nayo wakati wote. Ni furaha isiyotegemea maisha yako yapoje, ni furaha isiyotegemea una vitu gani bali ni furaha inayopatikana ndani mwako. Wengi hupata furaha kutokana na hali na vitu, na kipindi cha wakati mgumu wao hukosa furaha kwani furaha yao inategemea vitu vya nje ambavyo havidumu milele. Lakini katika meditation unajifunza kuachana na kujishikilia na mawazo, fikra, hisia, na milango ya ufahamu. Unajifunza kuingia ndani na kutafuta kisicho na mwanzo wala mwisho. Ambacho wakati wowote upo nacho, nacho kinakuunganisha source/chanzo na ufahamu mkuu wa Ulimwengu ambao wakati wote mpo pamoja.
9
18
156
52,049
BEYOND REASONABLE DOUBT Katika criminal jurisprudence, kuna kanuni moja ambayo haiwezi kupuuzwa, kupunguzwa wala kubadilishwa kwa sababu ya uzito wa shtaka, ambayo ni the prosecution must prove its case beyond reasonable doubt. Hiki sio kipimo cha kawaida cha ushahidi ila ni kiwango cha juu cha uthibitisho kinachotenganisha tuhuma na hatia, mashaka na hitimisho la kimahakama, pamoja na mamlaka ya Serikali ya kushtaki na wajibu wake wa kuthibitisha kosa. Maana yake ni kwamba Jamhuri haitoshi kuonyesha kuwa kuna uwezekano Lissu alitenda kosa. Lakini inapaswa kuwasilisha ushahidi unaoaminika, unaokubalika kisheria na wenye probative value ya kutosha kuthibitisha kila essential ingredient ya kosa linalodaiwa. Mahakama inapaswa kuridhika kwa kiwango cha kisheria kwamba ushahidi unaunga mkono hitimisho la hatia, bila kubaki na shaka yenye msingi inayotokana na rekodi ya shauri. Hapa kuna tofauti muhimu ambayo mara nyingi hueleweka vibaya, kwamba beyond reasonable doubt haimaanishi kutokuwepo kwa kila shaka inayoweza kufikiriwa. Sheria haitaki uhakika wa kihisabati, wala haidai Jamhuri ijibu kila nadharia ya kubuniwa. Lakini inachotaka ni kuondoa reasonable doubt shaka inayotokana na ushahidi, mantiki na mazingira halisi ya shauri. Shaka ya kubahatisha haina nguvu ya kisheria, lakini shaka inayotokana na contradiction ya msingi, pengo la ushahidi, kutokuthibitishwa kwa ingredient au ushahidi usioaminika haiwezi kufutwa kwa maelezo ya jumla. Katika kesi ya Lissu, kipimo hiki kinahitaji Mahakama kuchunguza kwa umakini mens rea yaani nia mahsusi inayodaiwa, actus reus yaani kitendo kinachounda kosa, tafsiri ya deed chini ya kifungu cha 39(2)(d). Attribution ya vitendo vinavyodaiwa na publication ya maneno kupitia Jambo TV. Haya ni maeneo tofauti ya kisheria yanayohitaji uthibitisho. Kwamba maneno yalitamkwa hakuthibitishi moja kwa moja nia ya uhaini, kwamba video ilisambazwa hakuthibitishi moja kwa moja nani aliyeichapisha. Na kwamba mkutano ulifanyika hakuthibitishi moja kwa moja kwamba ulikuwa na madhumuni ya kutenda kosa la uhaini. Hapo ndipo evidentiary nexus inapokuwa muhimu, yaani Mahakama inapaswa kuona uhusiano wa kimantiki na wa kisheria kati ya ushahidi uliowasilishwa na kila kipengele cha kosa. Haiwezi kuruka kutoka kwenye mazingira yanayotia shaka hadi kwenye hitimisho la hatia bila kuonyesha namna ushahidi unavyothibitisha kiungo hicho.
3
10
55
3,282
Katika ushahidi wa mazingira, chain of inference inapaswa kuwa thabiti, yaani ikiwa kuna pengo muhimu linaloacha maelezo mengine yenye msingi, Mahakama inapaswa kulichunguza badala ya kulifunika kwa dhana. Vilevile cumulative assessment of evidence haimaanishi kukusanya mashahidi wengi na kuhitimisha kwamba shtaka limethibitishwa. Inamaanisha kupima ushahidi wote kwa pamoja, huku kila kipande kikipewa uzito unaostahili kulingana na chanzo chake, uthabiti wake, uaminifu wa shahidi na uwezo wake wa kuthibitisha jambo husika. Credibility ya shahidi na probative value ya maelezo yake ni mambo yanayohusiana, lakini sio kitu kimoja. Shahidi anaweza kuwa na uwezo wa kutoa ushahidi, lakini Mahakama bado ikahitaji kuchunguza kama ushahidi wake unaaminika na una uzito wa kuthibitisha ingredient inayobishaniwa. Na hapa ndipo material contradictions zinapopata umuhimu, kwamba sio kila tofauti ya maelezo inavunja kesi. Lakini tofauti inayogusa utambulisho wa mtendaji, namna kitendo kilivyofanyika, chanzo cha taarifa au uhusiano wa mshtakiwa na tukio haiwezi kuchukuliwa kama kasoro ndogo bila uchambuzi. Mahakama inapaswa kujiuliza, tofauti hiyo inaathiri nini? Inadhoofisha reliability ya ushahidi kwa kiwango gani? Haya ndio maswali yanayofanya tathmini ya ushahidi kuwa kazi ya kimahakama, sio zoezi la kuhesabu mashahidi. Lakini kuna kanuni nyingine ambayo ni moyo wa haki ya jinai, kwamba the burden of proof never shifts to the accused. Lissu hana wajibu wa kuthibitisha kutokuwa na hatia. Hata kama utetezi haujajibu kila hoja ya Jamhuri, au kama ushahidi wa upande wa utetezi una mapungufu, hilo haliwezi kujaza mapengo ya mashtaka. Mahakama haiwezi kutoa conviction kwa sababu maelezo ya mshtakiwa hayajaridhisha pekee, ila lazima iridhike kwamba ushahidi wa mashtaka wenyewe umetimiza kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa. Hii ndio maana ya presumption of innocence, yaani sio kauli ya mapambo katika vitabu vya sheria, bali ni kinga ya kikatiba na ya kimahakama inayomzuia mtu kuhukumiwa kwa tuhuma, hisia, shinikizo la umma au tafsiri isiyothibitishwa. Kadiri shtaka linavyokuwa zito, ndivyo umuhimu wa Mahakama kuzingatia kwa makini viwango vya uthibitisho na uhalali wa kila ingredient unavyokuwa mkubwa. Na mwisho niseme, kuna ukweli mmoja wa kisheria unaopaswa kubaki wazi, kwamba reasonable doubt sio zawadi anayopewa mshtakiwa, wala sio upendeleo wa Mahakama. Lakini ni matokeo ya kushindwa kwa upande wa mashtaka kuthibitisha kosa kwa kiwango kinachotakiwa na sheria. Ikiwa ushahidi umethibitisha kila ingredient, sheria itoe matokeo yake. Ikiwa shaka yenye msingi imebaki kwenye ingredient muhimu, presumption of innocence lazima ipate maana yake halisi. Kwa sababu katika haki ya jinai, mtu hahukumiwi kwa kile ambacho huenda alikusudia kufanya, wala kwa kile ambacho wengine wanaamini alifanya. Ila anahukumiwa kwa kile ambacho Jamhuri imeweza kuthibitisha kisheria, na hapo ndipo mstari kati ya tuhuma na hatia unapochorwa. Sio kwa hisia, bali kwa ushahidi, sheria na reasonable doubt.
1
5
187
SIKU 1 KABLA YA HUKUMU YA LISU JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTlPAS LISSU, KESI YA JINAI NA. 19605/2025 Kesho ni siku ya hukumu, baada ya miezi ya kusikiliza ushahidi, kuchambua nyaraka, kuhoji mashahidi na kupima hoja za mawakili, safari hii ndefu ya kimahakama inafika kwenye kilele chake. Kwa Tundu Lissu, ni siku inayobeba uzito wa hatima yake. Kwa mfumo wa haki, ni wakati wa kuona namna sheria inavyotumika mbele ya shtaka zito kama uhaini. Lakini kabla ya Mahakama kutoa uamuzi, kuna swali ambalo linapaswa kubaki akilini mwa kila anayefuatilia shauri hili. Je, ushahidi umefikia kiwango cha kuthibitisha hatia, au uzito wa shtaka umeacha nafasi ya mashaka yenye msingi? Katika criminal jurisprudence, sio tuhuma zinazothibitisha kosa, ila ni ushahidi unaokidhi kila kipengele cha kisheria. Burden of proof iko kwa Jamhuri, na kiwango chake ni beyond reasonable doubt. Hii ndio nguzo inayolinda presumption of innocence. Narudia tena mshtakiwa hahitajiki kuthibitisha kutokuwa na hatia, wala Mahakama haiwezi kujaza mapengo ya ushahidi wa mashtaka kwa kutegemea udhaifu wa utetezi. Kwenye kesi hii, macho yako kwenye tafsiri ya kifungu cha 39(2)(d), uthibitisho wa mens rea, uwepo wa actus reus, maana ya deed, pamoja na uhusiano kati ya Lissu na kitendo cha uchapishaji kinachodaiwa. Haya ni masuala ambayo hayawezi kutatuliwa kwa hisia, msimamo wa kisiasa au tafsiri ya maneno nje ya mazingira yake. Yanahitaji strict construction of penal statutes, uchambuzi wa ushahidi na sababu za kimahakama zinazoweza kusimama mbele ya sheria. Pia kuna uzito wa credibility assessment, yaani Mahakama inapaswa kuangalia sio mashahidi walisema nini pekee, Bali walijuaje, walikuwa na nafasi gani ya kujua, maelezo yao yanaendana kwa kiwango gani, na contradictions zilizojitokeza zinaathiri vipi kiini cha shtaka.
8
45
179
7,936
Ushahidi wa mazingira nao unahitaji complete chain of inference, kwamba haiwezekani kuruka kutoka kwenye uwepo wa tukio hadi kwenye dhima ya mshtakiwa bila kuthibitisha uhusiano unaotakiwa kisheria. Lakini kesho, jambo muhimu zaidi halitakuwa kama Lissu atapatikana na hatia au la. Ila litakuwa pia namna Mahakama itakavyofafanua mpaka kati ya freedom of expression na criminal liability. Hotuba ya kisiasa inaweza kuwa kali, yenye ukosoaji mkubwa na hata yenye kuleta mvutano. Lakini, wajibu wa Mahakama ni kuamua kama ushahidi unaonyesha kosa lililofafanuliwa na sheria, na sio kuadhibu kauli kwa sababu tu zimezua mjadala. Na hapa ndipo hisia za kesi hii zinapokutana na ukali wa sheria. Nyuma ya jalada kuna binadamu, familia, wafuasi na jamii inayosubiri majibu. Lakini Mahakama haiwezi kuongozwa na huruma wala shinikizo la umma. Ila inapaswa kuongozwa na sheria na ushahidi. Haki ya kweli haichagui upande, ila inahakikisha kila mtu anapimwa kwa kiwango kilekile cha kisheria. Kesho, kila hoja itakuwa imefikishwa mwisho wake, walaa hakutakuwa tena na shahidi wa kuongeza maelezo, wala wakili wa kuwasilisha hoja mpya. Kutabaki ushahidi uliorekodiwa, sheria inayotumika na tafakari ya Mahakama. Na tunaposubiri, tukumbuke jambo moja muhimu sana, kwamba uhaini ni shtaka zito, lakini uzito wa shtaka hauwezi kuwa mbadala wa uthibitisho. Ikiwa kila ingredient imethibitishwa, sheria itumike, na ikiwa shaka yenye msingi inabaki kwenye kipengele muhimu, sheria hiyo hiyo inapaswa kulinda presumption of innocence. Kesho sio siku ya kelele, ila ni siku ya sababu za kimahakama. Sio siku ya hisia kushinda ushahidi, ila ni siku ya ushahidi kupimwa kwa sheria. Na kwa mtu anayesubiri hatima yake, tofauti kati ya tuhuma na uthibitisho sio tofauti ya maneno pekee, ila ni tofauti inayoweza kubeba maisha yake yote. KESHO, MAHAKAMA ITAZUNGUMZA. NA TUNACHOTARAJIA SI TU KUSIKIA UAMUZI, BALI KUELEWA SABABU ZA KISHERIA ZILIZOUFIKISHA HAPO.
1
7
348
UBUNIFU NA KUSHIRIKI KATIKA UWEPO Kuna tofauti kati ya kumiliki maisha na kushiriki katika kuyakuza. Tunapopanda mti, kuandika, kuchora, kuimba, kulea mtoto, kujenga, kuponya au kurejesha mazingira yaliyoharibika, tunashiriki katika mchakato wa kuleta kitu kipya duniani. Hatuanzi kutoka katika utupu kamili, ila tunatumia uwezo, nyenzo, maarifa na uwezekano ambao tayari upo katika ulimwengu. Ubunifu, kwa maana hii, ni mazungumzo kati ya mwanadamu na mazingira yake. Tunabadilisha ulimwengu, na ulimwengu huo huo hutubadilisha. Tunaunda vitu, lakini katika mchakato huo tunaunda pia namna mpya za kufikiri, kuhisi na kujielewa. Huenda kuwa mwanadamu mwenye ufahamu sio kuwa mtawala wa maumbile, bali kujitambua kama mshiriki mwenye wajibu katika mtandao wa uhai. Mti hauhitaji kuwa mwanadamu ili uwe na nafasi yake katika dunia. Mto hauhitaji kutambua thamani yake ili uwe sehemu ya mzunguko wa maisha. Na sisi hatuhitaji kujiona kuwa kitovu cha kila kitu ili maisha yetu yawe na maana. Uhusiano wetu na uhai hauhitaji msingi wa ubora juu ya viumbe vingine, bali utambuzi wa kutegemeana na wajibu wa kuhifadhi kile kinachotuwezesha kuishi. . . Mungu hunena katika kimya. Karibu kwenye WhatsApp channel yangu "Kimya Chenye Sauti" kwa tafakari na mahamasisho ya kiroho. whatsapp.com/channel/0029Vb5… #Imani #Tafakari #KimyaChenyeSauti
4
11
1,218
SIKU 2 KABLA YA HUKUMU YA LISU JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTlPAS LISSU, KESI YA JINAI NA. 19605/2025 Siku mbili kabla ya hukumu, tuangalie upande mwingine wa kesi hii. Safari hii sio kurudia mjadala wa mens rea na actus reus, Bali kujiuliza kama mnyororo wa ushahidi uliowasilishwa na Jamhuri una muunganiko wa kutosha kumhusisha Lissu na kosa linalodaiwa. Katika sheria ya ushahidi, kuna tofauti kubwa kati ya kuthibitisha kwamba tukio lilitokea na kuthibitisha kwamba mshtakiwa ndiye anayewajibika kwa tukio hilo. Kwamba mkutano ulifanyika, maneno yalitamkwa na matangazo yalirushwa moja kwa moja, hakujibu moja kwa moja swali la nani aliandaa mkutano, Nani aliwaalika waandishi na nani alifanya kitendo cha uchapishaji kinachodaiwa. Hapa ndipo attribution of criminal responsibility inakuwa muhimu. Jambo jingine la kutazamwa ni evidentiary gaps, kwamba ushahidi wa shahidi mmoja unapopingana na wa mwingine kuhusu jambo muhimu, Mahakama haiwezi kuishia kusema kuwa tofauti ni za kawaida. Inapaswa kuchunguza chanzo cha tofauti hizo, athari zake kwenye hoja ya mashtaka na kama ushahidi mwingine huru unaziondoa. Hasa pale ambapo tofauti zinahusu kitendo kinachodaiwa kuwa msingi wa kosa, uzito wake haupaswi kupuuzwa. Pia kuna suala la circumstantial evidence, yaani Jamhuri inaweza kutegemea ushahidi wa mazingira, Lakini mazingira hayo yanapaswa kuunda mnyororo wa inference unaoelekea kwenye hitimisho la hatia bila kuacha maelezo mengine yenye msingi.
6
15
82
5,014
Uwepo wa Lissu kwenye mkutano, kauli zake na matangazo ya vyombo vya habari ni mazingira yanayopaswa kuchunguzwa. Lakini kila moja linahitaji kuunganishwa na ingredient husika ya kosa. Na hapa mahakama inapaswa kujilinda dhidi ya kufanya inference moja kuwa ushahidi wa kila jambo. Tuzungumzie pia burden of proof, katika shauri la jinai, mshtakiwa hahitajiki kujibu kila pengo la ushahidi wa mashtaka kwa kutoa maelezo mbadala. Jamhuri ndio yenye wajibu wa kuthibitisha shtaka, hata kama baadhi ya ushahidi wa utetezi unaweza kuwa na mapungufu, hilo haliongezi nguvu ya ushahidi wa mashtaka moja kwa moja. Kanuni ni moja, kwamba kesi hupimwa kwa nguvu ya upande unaobeba mzigo wa uthibitisho, na sio kwa udhaifu wa upande unaojibu tuhuma. Pia niwajuze kitu kwamba kuna jambo ambalo linaweza kuamua namna hukumu itakavyosomwa, yaani judicial reasoning. Umuhimu wa hukumu hautakuwa kwenye sentensi ya mwisho pekee, bali katika namna Mahakama itakavyochambua kila ingredient, kushughulikia contradictions, kutafsiri kifungu cha 39(2)(d) na kueleza kwa nini ushahidi fulani umekubalika au umekataliwa. Hapo ndio tutakapoweza kuona kama hitimisho limejengwa kwa misingi thabiti ya sheria na ushahidi. Tunakaribia siku ya majibu, lakini katika kesi hii, swala la msingi sio kama Jamhuri imeonyesha kwamba kulikuwa na maneno yenye utata au mazingira yenye mvutano wa kisiasa. Ila ni kama imeunganisha mazingira hayo na kila sharti la kosa la uhaini kwa kiwango cha beyond reasonable doubt. Tulumbuke pia katika sheria ya jinai, mnyororo wa ushahidi hauwezi kuwa na kiungo kinachokosekana halafu hitimisho likachukuliwa kuwa limekamilika. Ijumaa, macho yatakuwa kwenye namna Mahakama itakavyopima mnyororo huo.
1
2
7
335
SIKU 3 KABLA YA HUKUMU YA LISU JAMHURI DHIDI YA TUNDU ANTlPAS LISU, KESI YA JINAI NA. 19605/2025 Siku tatu pekee zimetutenganisha na hukumu katika kesi hii ya uhaini Baada ya kusikiliza mashahidi 17 wa upande wa mashtaka, mashahidi watano wa utetezi na hoja za mwisho za pande zote, Sasa Mahakama inakabiliwa na jukumu la kutoa majibu ya kisheria kuhusu tuhuma nzito zinazomkabili Tundu Lissu. Lakini kuna jambo moja ambalo tusilipoteze, swali sio kama Lissu alitamka maneno yanayobishaniwa, Ila swali ni kama Jamhuri imethibitisha kwamba maneno hayo yanatimiza kila ingredient ya kosa la uhaini. Hapo ndipo vita halisi ya kisheria ilipo. Jamhuri imejenga hoja yake kwenye tafsiri ya maneno, nia iliyodaiwa na namna ujumbe ulivyofikishwa kwa umma. Utetezi umejikita kwenye mazingira ya kisiasa, mapengo ya ushahidi na tofauti za maelezo ya mashahidi. Mahakama sasa inapaswa kutenganisha hotuba kali ya kisiasa na kitendo kinachounda kosa la jinai, tukumbuke sio kila kauli inayoweza kutafsiriwa kuwa tishio inakuwa moja kwa moja uhaini. Kwenye mens rea, swali ni kama ushahidi unaonyesha nia mahsusi ya kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi kwa madhumuni ya kuitisha Serikali, au kama hitimisho hilo limejengwa zaidi kupitia tafsiri ya maneno. Kwenye actus reus, mjadala ni kama kutamka na kusambaza maneno kunatimiza dhana ya deed chini ya kifungu cha 39(2)(d). Kisha kuna attribution, kwamba ni nani aliandaa mkutano, nani aliwaalika waandishi wa habari na nani alichapisha video. Tofauti za ushahidi kuhusu masuala haya zina uzito pale zinapogusa kitendo kinachodaiwa kufanywa na mshtakiwa. Kutamka ujumbe, kujua kuwa unarekodiwa na kufanya kitendo cha kuuchapisha sio lazima yawe jambo moja kisheria.
5
13
138
9,383
Mahakama inapaswa kuchunguza kama ushahidi unaunganisha hatua hizo bila kutegemea dhana zisizothibitishwa. Hata kuhusu mashahidi, idadi yao sio kipimo cha mwisho. Kinachohesabika ni credibility, consistency na probative value. Yaani kama mashahidi walikuwa na maarifa ya moja kwa moja, maelezo yao yanaendana, tofauti zilizojitokeza ni za pembeni au zinagusa kiini cha shtaka, Na pale shahidi anapokuwa na maslahi binafsi katika matokeo ya shauri, je mazingira hayo yamezingatiwa katika kupima uzito wa ushahidi wake. Lakini kuna kipimo kimoja kinachozidi hoja zote, beyond reasonable doubt. Jamhuri ilipaswa kuthibitisha kila ingredient muhimu ya kosa. Lissu hana wajibu wa kuthibitisha kutokuwa na hatia. Ikiwa shaka yenye msingi inabaki kwenye nia, kitendo au uhusishaji, Mahakama inapaswa kuikabili kwa mujibu wa kanuni ya presumption of innocence. Hii ndio sababu hukumu hii ina uzito unaozidi hatima ya mshtakiwa mmoja. Inagusa mpaka kati ya uhuru wa kujieleza, ushindani wa kisiasa na dhima ya jinai. Mahakama inapaswa kutoa sababu zinazoonyesha namna ilivyotafsiri sheria na kupima ushahidi, na sio kutangaza hukumu pekee. Ijumaa tunasubiri majibu ya Mahakama kuhusu jambo moja, kwamba jamhuri imeondoa mashaka yenye msingi kuhusu kila ingredient ya uhaini, au bado kuna pengo kati ya kile kinachodaiwa na kile kilichothibitishwa kisheria. Mwisho wa yote, uzito wa shtaka hauwezi kuchukua nafasi ya uzito wa ushahidi. Na katika sheria ya jinai, hatia lazima ithibitishwe haiwezi kudhaniwa.
1
5
403
KUACHILIA NI UHURU USIOHITAJI UMILIKI Kuna aina ya mateso yanayotokana na kujaribu kuufanya ulimwengu udumu katika hali ambayo tayari imeanza kubadilika. Tunashikilia utambulisho ambao tumeuzoea, mahusiano ambayo yamebadilika, matarajio ambayo hayakutimizwa na kumbukumbu ambazo tunatamani zingeweza kurudi. Wakati mwingine, tunachokiogopa sio kupoteza kitu pekee, bali ni kupoteza namna tulivyojielewa kupitia kitu hicho. Lakini hakuna umbo la maisha linaloweza kusimama milele katika hali ileile. Kuachilia ni kutambua kwamba thamani ya jambo fulani haihitaji kulimiliki milele, na kwamba upendo hauhitaji kumfunga mwingine ili uthibitike.
1
7
35
1,623
Tunaweza kupenda bila kumiliki na tunaweza kukumbuka bila kuishi ndani ya yaliyopita. Pia tunaweza kuheshimu tulivyokuwa bila kulazimisha maisha ya sasa yaendelee kufuata sura ya zamani. Kuachilia sio kutojali, wala sio kukwepa wajibu ila ni kutambua tofauti kati ya kile tunachoweza kukitunza na kile ambacho hakiwezi kubaki chini ya matakwa yetu. Na hapa ndipo uhuru wa ndani unapoanza, na sio katika uwezo wa kuamuru kila jambo litokee tunavyotaka, bali katika uwezo wa kuchagua namna tutakavyokabiliana na yale ambayo hatuwezi kuyabadilisha. . . Mungu hunena katika kimya. Karibu kwenye WhatsApp channel yangu "Kimya Chenye Sauti" kwa tafakari na mahamasisho ya kiroho. whatsapp.com/channel/0029Vb5… #Imani #Tafakari #KimyaChenyeSauti
1
2
139
RIP, Alute Lissu Mughwai kifo kimehitimisha legal personality yako, lakini hakiwezi kufuta heshima, utu na urithi wako. Mwenyezi Mungu akupokee katika rehema zake. Requiescat in pace, Pumzika kwa amani 🕊
20
142
2,612
HOTUBA YA LEMA NA ISHARA ZILIZOJIFICHA NYUMA YA UJUMBE WA MARIDHIANO Jana, tarehe 1 November 2026, Godbless Lema alikutana na waandishi wa habari pale Kibo Palace Hotel jijini Arusha. Nilipoanza kuichambua hotuba yake, niliona kwamba haikupaswa kusomwa kwa haraka kama taarifa nyingine za kawaida za kisiasa. Kulikuwa na ujumbe wa wazi, lakini pia kulikuwa na maeneo ambayo yalihitaji deeper intelligence scrutiny. Sikujikita kwenye maneno aliyoyasema pekee, ila nilianza kuchunguza timing, context, target audience, strategic intent na uwezekano wa athari za ujumbe huo ndani ya CHADEMA. Katika taaluma ya kivuli, tunajua kwamba wakati mwingine uzito wa taarifa haupo kwenye maneno yenyewe, bali kwenye sababu zilizomfanya mtu ayaseme, wakati aliyoyasema na watu aliotaka wayasikie. Jambo la kwanza lililonivutia lilikuwa msisitizo wake kwamba mazungumzo hayakuwa usaliti. Lema alilijenga suala hili kwa nguvu, akisisitiza kwamba CHADEMA ilikuwa taasisi ya kisiasa na kwamba mawasiliano na Serikali au vyombo vya dola yasingepaswa kutafsiriwa moja kwa moja kama kusaliti misingi ya chama. Hapa nilianza kufanya kile tunachokiita message deconstruction, yaani kuvunja ujumbe katika vipengele vyake ili kuelewa kilichokuwa kinasisitizwa na kwa nini. Kwa nini dhana ya usaliti ilipewa nafasi kubwa kiasi hicho? Je, kulikuwa na hofu ya ndani ambayo alitaka kuiondoa? Je, alikuwa akijaribu kupima receptivity ya wanachama kuhusu wazo la maridhiano? Au ujumbe wake ulikuwa umeelekezwa kwa watu ambao huenda walikuwa na mashaka kuhusu mabadiliko ya mbinu za kisiasa? Sikupata jibu la moja kwa moja, lakini niliona uwezekano wa perception management, yaani kuandaa mazingira ya namna hadhira itakavyopokea na kutafsiri wazo fulani. Kisha nikafika kwenye sehemu iliyohusu Freeman Mbowe. Lema alisimulia mazungumzo aliyodai kufanya na Mbowe katika hafla ya harusi, akisema Mbowe alimweleza kwamba alikuwa ameamua kustaafu siasa. Pia alieleza kwamba alifikisha taarifa hiyo kwa John Mnyika na kupendekeza Mbowe aondolewe kwenye kundi la mawasiliano la chama, lakini pendekezo hilo halikukubaliwa. Hapa niliona kile ambacho katika intelligence assessment tungekiita significant information disclosure. Yaani kwa nini mazungumzo ya faragha kuhusu mustakabali wa kiongozi mwenye ushawishi ndani ya chama yaliwekwa hadharani katika mkutano uliokuwa unazungumzia maridhiano. Je, ilikuwa ni contextual disclosure, yaani kutoa historia ya mawasiliano ili kueleza msimamo wake, au taarifa hiyo ilikuwa na athari nyingine katika mjadala wa mamlaka na ushawishi ndani ya chama. Niliona kwamba maelezo hayo yangeweza kubadili internal perception kuhusu nafasi ya Mbowe, lakini sikuwa na ushahidi wa kusema hilo ndilo lilikuwa lengo lake. Na hapa ndipo mchambuzi makini anapaswa kutenganisha observable facts na analytical inference. Jambo la pili lililonifanya niongeze umakini lilikuwa namna ujumbe wa maridhiano ulivyohusishwa na hoja ya kujenga taasisi. Kwa mtazamo wa strategic positioning, lugha aliyotumia Lema ingeweza kutafsiriwa kama jaribio la kuipa nafasi mbinu ya mazungumzo ndani ya mazingira, Ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yamejengwa zaidi kwenye shinikizo la kisiasa na mapambano ya hadharani. Hapa nilijiuliza maswali mawili, kwamba alikuwa akitetea mbinu ya ziada inayoweza kuambatana na mapambano ya kisiasa, au alikuwa akifungua mlango wa strategic realignment, yaani mabadiliko ya mwelekeo wa kimkakati. Hapa naweza kusema tofauti yake ilikuwa kubwa, yaani mbinu zinaweza kubadilika bila kubadilisha misingi, lakini mabadiliko ya mkakati yanahitaji uhalali, mamlaka na uwajibikaji wa kitaasisi.
5
28
148
11,824
Ya tatu ilikuwa kwamba hotuba yake ilikuwa imeakisi tofauti za mitazamo zilizokuwepo ndani ya CHADEMA kuhusu uongozi, mamlaka na mustakabali wa mkakati wa kisiasa. Lakini hakuna hata mojawapo niliyo ithibitisha, ila kwangu mimi, thamani ya nadharia hizi imekuwa katika kutuonyesha ni taarifa zipi tunahitaji kuzitafuta ili kupata picha iliyo sahihi zaidi. Baada ya press ile, niliona umuhimu wa kufuatilia early warning indicators, yaani kuangalia kama John Mnyika, Freeman Mbowe au wajumbe wa Kamati Kuu wangetoa ufafanuzi. Lakini sikuona hilo Lakini swali lililobaki akilini mwangu npaka sasa ni hili, kwa nini umuhimu wa mazungumzo ulielezwa kwa msisitizo mkubwa kuliko maelezo ya mamlaka, ajenda, wahusika na masharti yake Naweza kusema hapo ndipo intelligence gap ilipojitokeza. Pengo la taarifa halikuwa ushahidi wa njama, lakini lilikuwa eneo ambalo lilihitaji ufafanuzi. Nimeona kwamba kama mchakato huo ungekuwa na manufaa kwa chama na taifa, basi uwazi kuhusu misingi yake ungeimarisha uaminifu na kupunguza tafsiri zinazoweza kuleta migawanyiko. Niseme tena tathmini yangu baada ya mkutano wa jana ni kwamba hotuba ya Lema imefungua mjadala mkubwa kuliko ule ulioonekana juu ya uso wake. Imehalalisha dhana ya mazungumzo, imeingiza tena suala nyeti la Mbowe katika mjadala wa umma na imeibua maswali kuhusu mamlaka na mwelekeo wa kisiasa wa CHADEMA. Sijapata ushahidi wa kutosha wa kusema Lema alikuwa amenunuliwa, ametumwa na mtu au kulikuwa na operesheni ya siri ya kukigawa chama. Lakini niliona indicators ambazo hazipaswi kupuuzwa, na niliona information gaps ambazo zilihitaji majibu.
2
3
6
602
Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na mashaka na kuwa na ushahidi. Katika intelijensia, tunasema suspicion initiates inquiry and evidence supports assessment. Mashaka yanaweza kuanzisha uchunguzi, lakini ushahidi ndio unaojenga hitimisho. Ndio maana sijaona busara ya kumhukumu Lema kwa hisia, wala sijaona busara ya kupuuza maswali yaliyojitokeza kutokana na hotuba yake. Na hapa ndipo nilipobaki na swali ambalo ningependa nawe ulitafakari. Ni kweli Lema alikuwa anatetea mazungumzo kama njia ya kutafuta suluhisho pekee, au hotuba yake imeanza kuandaa mazingira ya kisiasa kwa ajili ya mabadiliko mapana zaidi ya mkakati ndani ya CHADEMA? Lakini jambo moja lilikuwa wazi hotuba ya jana tayari imeweka ujumbe mezani na kilichofuata ndicho kimeonyesha uzito wake halisi. Katika lugha ya kivuki, hatuangalii tukio moja pekee, ila tunafuatilia signals, patterns, actors, motives, capabilities, opportunities na kufikia outcomes. Kwa sababu wakati mwingine mabadiliko ya kisiasa hayaanzi kwa tangazo kubwa, Ila huanzia kwenye lugha ambayo hujengwa kupitia mitazamo kisha huimarishwa na mawasiliano, na baadaye huonekana kwenye maamuzi. Na hapo ndipo picha nzima huanza kujifunua. Mwisho, strategic timing ya hotuba hii imekuwa kiashiria kingine muhimu. Lema ameitoa jana, siku chache kabla ya hukumu ya Tundu Lissu, katika kipindi ambacho political environment ilikuwa nyeti sana. Ukaribu huu wa matukio unaifanya hotuba yake kuwa na uzito wa ziada katika situational assessment, hasa kwa kuzingatia ujumbe wake kuhusu mazungumzo na Serikali. Sisemi kuwepo kwa operational linkage kati ya matukio hayo, lakini timing, context and messaging vimeacha maswali muhimu kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa CHADEMA na mazingira mapana ya upinzani. Niwakumbushe jambo moja muhimu kwamba, katika intelligence, muda wa tukio ni sehemu ya uchambuzi, na sio uthibitisho wa njama, bali ni indicator inayostahili kuzingatiwa. BYE
2
2
4
469
Binafsi nilijifunza kung'amua jema kwenye kila baya, pakikucha na mimi nitasema utata nilisikia kwenye press ya kaka Lema, japo siasa zinaumiza sana. Aluta Continua ✌🏾
1
11
135
3,025
Paul Bonaventure retweeted
SALAMU ZA POLE
7
93
374
4,527
Twaha Mwaipaya lazima apatikane akiwa alive and safe. Yeyote aliyehusika, directly or indirectly, awajibishwe kwa mujibu wa sheria. No one is above the law, no institution is above accountability.
4
45
184
4,018
Paul Bonaventure retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia. Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama. Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki. Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa. Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo. Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo. Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe. Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni. 1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote. 2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela. 3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi. 4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia. 5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake. 6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu. 7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu. 8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini. Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo… Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii. Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa. Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote. Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
82
737
12
2,256
31,826