Mnyama amekuja kivingine! Kuanzia jezi ya bluu, nyeupe hadi nyekundu, kila moja ina upekee wake. Ubunifu, muonekano na mchanganyiko wa rangi umeifanya jezi hii kuwa gumzo.
Je, ubora huu unaweza kuwaunganisha Wanasimba na kuwafanya wasahau tofauti zao kwa muda? 馃槀
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amewataka wananchi wa Katoro, mkoani Kagera, kulinda amani kwa vitendo na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA), Godbless Lema, ametoa wito mzito kwa wananchi, maaskofu, na mashehe nchini kuamka na kulinda viongozi wao dhidi ya dhuluma za kisiasa, huku akisisitiza kuwa chama hicho hakijawahi wala hakikusudii kupanga uasi au fujo nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, akielezea kuhusu uchaguzi wa Klabu ya Simba SC unaotarajiwa kufanyika Januari 2027.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, ametoa wito mzito kwa wananchi kujiepusha na fikra za chuki na kulipiza kisasi, akisisitiza kuwa njia ya chuki haijawahi kuwa suluhu ya matatizo ya kisiasa au uonevu nchini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia wizara, halmashauri na taasisi mbalimbali za kifedha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara Ally Gugu, ameshiriki Ibada ya Mazishi ya Deusdedit Mwita Wambura, ambaye ni Baba Mzazi wa Mkuu Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura yaliyofanyika Musoma Mkoani Mara.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, ameweka wazi msimamo wake mzito kuhusu mustakabali wa chama hicho, akisisitiza utayari wake wa kushuka na kuwa mdogo kwa ajili ya kulinda uhai wa chama.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amesisitiza kuwa harakati na kazi ya upinzani nchini si kwa ajili ya kutafuta utukufu binafsi, bali ni wajibu mkubwa wa kutafuta mabadiliko ya nchi.
Viongozi wa klabu ya Simba Mkoa wa Mwanza wamejitokeza hadharani kutoa tamko la kuunga mkono mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 3, 2027 huku wakionyesha kutokuridhishwa na mienendo ya mwenyekiti wao wa klabu hiyo, Muktaza Mangungu.
Dkt. Vincent Lissu Mughwai, Msemaji wa Familia ya kina Lissu, amesema shughuli za maziko ya Mzee Alute Mughwai Lissu aliyefariki usiku wa kuamkia leo, Jumapili Novemba 01.2026 yatafanyika baada ya HUKUMU ya mdogo wake ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu kutolewa.
Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Kagera, Leodger Kachebonao 'Mendez' amempongeza Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Faris Buruhani kwa heshima aliyoiletea Kagera kupitia uteuzi wake akisema hatua hiyo imewapa furaha na kujivunia kuwa na kijana kutoka mkoani humo aliyefikia nafasi
Breaking News:
Taarifa zilizotufikia hivi punde (leo, Jumapili Novemba 01.2026) zinaeleza kuwa Kaka yake Tundu Lissu (Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa), Mzee Alute Mughwai Lissu (Wakili) amefariki Dunia
Dada yake Tundu Lissu, Mchungaji Rose amethibitisha kutoka taarifa hiyo...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amewataka viongozi na watendaji wa Serikali kuhakikisha wananchi, hususan vijana, wanafanya shughuli zao za kiuchumi bila kusumbuliwa na watu wanaotumia vibaya madaraka yao.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Faris Buruhani, amewataka viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kagera kuchukua hatua dhidi ya watu wanaodaiwa kutumia vibaya dhamana waliyopewa ya kudhibiti magendo ya kahawa, badala yake kuwatoza fedha wananchi wanaosafirisha kahawa zao.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mwanga na Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA Taifa, Lembrus Mchome, amepinga hatua ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, kutangaza mpango wa kugoma kula, akisema hatua hiyo inaweza kuhatarisha afya yake.
Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, ameeleza hatua zilizofikiwa katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, akisema katiba mpya imekamilika na kinachosubiriwa ni kukamilika kwa usajili wa Baraza la Wadhamini kabla ya kuendelea na hatua nyingine.
Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema mchakato wa mabadiliko ya uongozi wa klabu hiyo una taratibu zake ambazo lazima zifuatwe na mamlaka husika.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imefanikiwa kujenga na kukamilisha miundombinu muhimu katika Mji wa Serikali Mtumba kwa kutumia fedha zake yenyewe bila msaada kutoka taasisi yoyote.



