EVENING WORD
SERMON: THE WORD OF GOD REMOVES IGNORANCE
The Word of God removes the ignorance within a person. The more you learn and meditate on His Word, the more your mind is renewed and your character is transformed.
When you fast and pray, having been firmly grounded in the Word of God, you increasingly reflect the image and character of God in your life. Seek to understand what the Word of God says concerning the challenges you are facing. Every question and challenge you encounter here on earth has an answer in His Word.
© Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira
8
NENO LA JIONI
SOMO: NENO HUONDOA UJINGA
Neno la Mungu huondoa ujinga uliomo ndani ya mtu. Unavyojifunza na kutafakari, ndivyo mawazo yako yanavyofanywa upya na tabia za hubadilishwa.
Unapofunga na kuomba ukiwa umejengwa katika Neno la Mungu, unazidi kuakisi sura na tabia ya Mungu katika maisha yako. Tafuta kulijua Neno la Mungu kwa habari ya hiyo changamoto unayopitia. Kila swali na changamoto unayopitia hapa duniani kuna jibu katika Neno lake.
© Mtume na Nabii josephat Elias Mwingira
9
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira — Kanisa la Efatha
TAREHE: 19/11/2026
SOMO: UIMARISHWE NA NGUVU YA YESU
Kuwa na Yesu hakumaanishi kwamba umemaliza kila kitu. Ruhusu nguvu yake ikuimarishe kwa ndani. Hapo ndipo unapoanza kutembea katika mamlaka aliyokupa ya kukanyaga nyoka na nge. Ibilisi asikusumbue wala asikuchezee. Wachawi wasikukaribie, wala waganga wasije kukuagua.
Utakapokutana na Mungu wa miungu, kila mtu atatambua kwamba umekutana naye. Mabadiliko yataonekana katika maisha yako.
Nia ya moyo wako itakusukuma kuleta mabadiliko. Inategemea umesikia nini na umeelewa nini. Anza kwa kutendea kazi kile ulichosikia na kukielewa. Hapo ndipo utaanza kuona kinapokupeleka.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira — Efatha Church
DATE: 19/11/2026
SERMON: BE STRENGTHENED BY THE POWER OF JESUS
Having Jesus in your life does not mean your work is done. Let His power strengthen you from within. Then you will begin to walk in the authority He has given you to trample on snakes and scorpions. Do not let the devil trouble you or toy with you. Let no witch come near you and no diviner come to tell your fortune.
When you encounter the God of gods, everyone will know you have met Him. They will see the change in your life.
The resolve in your heart will move you to bring about change. It depends on what you have heard and understood. Begin by putting what you have heard and understood into practice. Then you will begin to see where it leads you.
31
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.
Hakutakuwa na kubangaiza Chakula au kulala njaa katika Nyumba yangu. Mimi nitakula Vinono, Mimi Nimebarikiwa na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
DECLARATION OF THE DAY.
I BLESS MY THURSDAY.
There shall be no lack of Food, nor shall anyone go hungry in My Home. I shall eat the Finest of Foods; I am Blessed by the LORD.
Thank You, JESUS. Thank You, Lovely Heavenly FATHER. Thank You, HOLY SPIRIT.
1
48
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.
Hakutakuwa na kubangaiza Chakula au kulala njaa katika Nyumba yangu. Mimi nitakula Vinono, Mimi Nimebarikiwa na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
EVENING WORD
SERMON: INTERPRETATION OF DREAMS
The gift of interpreting dreams enriches a person's salvation and helps build the love of God within them. When you have this gift, you will love God, and whenever He speaks, you will be able to hear His voice because of your love for Him. When you understand how to interpret dreams, it becomes much easier for you to experience the goodness of God.
The goodness of God is constantly at work, but many people fail to experience it because they do not understand how to interpret it. If you fail to understand the meaning of your dream, you may miss the opportunity to respond appropriately. To understand God's messages and the dreams you receive, you need to have the Spirit of God within you to guide and help you.
©️ Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira
1
71
NENO LA JIONI
SOMO: TAFSIRI YA NDOTO
Kipawa kwa ajili ya waota ndoto hupendezesha wokovu wao na kujenga upendo wa Mungu ndani yao. Ukiwanacho utampenda Mungu na wakati wote utakapokuwa akisema utamsikia kwa sababu unampenda. Ukijua kutafsiri ndoto ni rahisi sana kwako kupata wema wa Mungu.
Mara zote wema wa Mungu hutembea lakini watu hawaupati kwa sababu hawaelewi tafsiri yake. Usipoelewa tafsiri ya ndoto yako utashindwa kuitikia. Ili uweze kuelewa ujumbe wa Mungu na ndoto unazoota ni lazima uwe na Roho wa Mungu ndani akusaidie.
©️ Mtume na Nabii josephat Elias Mwingira
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 18/11/2026
SOMO: USIKUBALI KUSHINDWA
Maisha ya wokovu ni maisha ya uaskari, sio maisha ya lelemama au ulegelege. Ni maisha ya mtu aliadhamiria kwenda mbele. Unapokabiliwa na dhambi, aibu au kushindwa, usiseme, “Mimi siwezi.” Sema, “Bwana, nitie nguvu niweze kushinda.”
Katika kutafuta ushindi wako, usijitiishe chini ya ufalme wa giza wala kukubali kutawaliwa na dunia. Amka, simama imara, upige vita vizuri vya imani, kama Neno linavyotuagiza katika 1 Timotheo 6:12.
Hata jambo linapoonekana kuwa gumu kulishinda, usiseme, “Nimeshindwa.” Mwambie Bwana, “Nitie nguvu, unipe ushindi.” Kumbuka neno hili la Wafilipi 4:13, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
Ita usaidizi, lakini usisalimu amri, hatakama changamoto hiyo inakuzidi umri, yupo aliye na umri mkubwa kuliko hilo tatizo.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 18 November 2026
SERMON: REFUSE TO ACCEPT DEFEAT
The life of salvation is the life of a soldier. It calls for discipline and a determination to press forward. When you face sin, shame, or failure, do not say, “I can’t.” Say, “Lord, give me the strength to overcome.”
As you seek victory, refuse to submit to the kingdom of darkness or let the world rule over you. Rise up, stand firm, and fight the good fight of faith, as the Word instructs us in 1 Timothy 6:12.
Even when something seems hard to overcome, do not say, “I’ve been defeated.” Tell the Lord, “Strengthen me and give me victory.” Remember these words from Philippians 4:13, “I can do all things through Him who strengthens me.”
Call for help, but do not surrender. Even if that challenge is older than you, there is One who is older than the challenge itself.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATANO YANGU.
Mimi nitakopesha maana nitakuwa na UTELE. Mimi Nimebarikiwa na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
DECLARATION OF THE DAY.
I BLESS MY WEDNESDAY.
I shall lend, for I will walk in ABUNDANCE. I am Blessed by the LORD.
Thank You, JESUS. Thank You, Lovely Heavenly FATHER. Thank You, HOLY SPIRIT.
4
97
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 17/11/2026
SOMO: MJUE MUNGU KWANZA
Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani. Ndivyo mema yatakavyokujia.”
Mahitaji yako yatatimizwa na Mungu baada ya kumjua Yeye. Watu wengi hujishughulisha kutafuta fedha ili wawe vile wanavyotamani kuwa, lakini hawatengi muda wa kutosha kumtafuta Mungu.
Kadiri unavyomfahamu Mungu, ndivyo unavyopokea kile ambacho ni stahiki yako. Kwa jinsi unavyomfahamu, kwa kiwango hicho hicho utapokea kile ambacho ni stahiki yako.
Siku utakapoelewa kwamba Mungu ndiye aliyekuumba na kukuweka katika bustani aliyoipanda ili uitunze, ndipo utakapofahamu kwamba wewe ni tajiri. Akili yako ikiendelea kukuambia kwamba wewe ni maskini, fikra hizo zitakuzuia kufikia hatua ambayo Mungu alikuumbia uifikie.
Chochote unachomiliki, unakimiliki kwa niaba ya Muumbaji. Yeye ndiye aliyeviumba vyote, nawe amekukabidhi jukumu la kuvitunza.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 17/11/2026
SERMON: GET TO KNOW GOD FIRST
Job 22:21 “Get to know God well, so that you may have peace. Then good things will come to you.”
As you come to know God, He will meet your needs. Many people keep themselves busy pursuing money so they can become who they want to be, but they set aside too little time to seek God.
The more you know God, the more you receive what is rightfully yours. What you receive is in proportion to how well you know Him.
The day you understand that God created you and placed you in the garden He planted so you could tend it, you will realize that you are rich. If your mind keeps telling you that you are poor, those thoughts will keep you from reaching the place God created you to reach.
Whatever you own, you hold on behalf of the Creator. He created it all and entrusted you with the responsibility of caring for it
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMANNE YANGU.
Upendo wa BWANA umetuzunguka, Familia yangu ni Salama, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo, wala ukata. Mimi na Familia yangu TUMEBARIKIWA na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATATU YANGU.
Mimi ni Mshindi siwezi kushindwa. Mjini sitashindwa, Vijijini sitashindwa. Mimi NIMEBARIKIWA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
Kuna mengi yamechukua muda wako wiki hii; Jumapili hii, tenga muda wa kuwa nyumbani mwa Bwana.
Tunakukaribisha kesho, tarehe 15 Novemba 2026, saa 2:00 asubuhi, Efatha Church Mwenge, Dar es Salaam.
Mpe Mungu nafasi ya Kwanza, Usichelewe Ibadani.
#EfathaChurch
#SundayService
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira — Kanisa la Efatha
TAREHE: 14/11/2026
SOMO: KUWAHI IBADANI.
Zaburi 122:1 “Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.”
Furaha ya kuwahi ibadani huleta neema ya kipekee kutoka kwa Mungu. Wanaompenda Mungu huona fahari kuwa katika nyumba yake mapema. Watu wa dunia hutegemea magari na farasi, lakini wana wa Mungu hulitumainia jina la Bwana.
Bwana Yesu alisema kulikuwa na wanawali kumi ambapo watano walikuwa na hekima na watano walikuwa wapumbavu. Wenye hekima walikuwa na mafuta yao lakini wapumbavu walikuwa hawana mafuta. Alipofika Bwana harusi wao ikabidi wakimbie kutafuta mafuta na waliporudi wakakuta wamechelewa na mlango umefungwa.
Unaweza kuwa mwaminifu katika kazi yako, biashara au masomo, lakini inapokuja katika mambo ya Mungu unachelewa. Mwana wa Mungu, usichelewe Kanisani, maana katika mkutano wa watakatifu, Mungu ndiye mwenyeji na mkuu wa mkutano. Kuchelewa ni ishara ya kutomheshimu Mungu na kusababisha wewe uchelewe kupokea. Inaweza kuonekana ni jambo dogo, lakini kuna Baraka ya kipekee kwa wanaowahi kwa sababu Mungu anaona heshima yako, naye atakuheshimu pia.




























