TCAA inafanya tathmini ya kiufundi ya huduma za uongozaji ndege ikijikita katika viashiria na malengo ya usalama, usimamizi wa mtiririko wa ndege, utekelezaji wa miradi na udhibiti wa vihatarishi, kupitia kikao kazi kinachofanyika Kibaha, Novemba 19–20, 2026.
#TCAA #usafiriwaanga
Tanzania na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) zimefanya mazungumzo kuhusu kuimarisha huduma za uongozaji ndege, usalama wa usafiri wa anga na ushirikiano wa kiufundi, kando ya Mkutano wa ATConf/7 unaofanyika jijini Montréal, Canada.
#TCAA #ICAO #usafiriwaanga
TCAA imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya utendaji bora kwa taasisi za usimamizi chini ya Wizara ya Uchukuzi.
Tuzo hiyo imekabidhiwa Novemba 17, 2026, na Naibu Waziri, Dkt. Switbert Mkama, na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Bi. Mtumwa Ameir, Mwanza. #TCAA
Tanzania is participating in ICAO’s Seventh Worldwide Air Transport Conference (ATConf/7), held in Montréal, Canada, from 16–20 November 2026, advocating stronger aviation connectivity, sustainable growth and enhanced support for developing States.
#ICAO #TCAA #usafiriwaanga
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mha. Flora Alphonce, aliwasilisha mada kuhusu utendaji wa sekta kwa mwaka 2025/26.
Mkutano huo unalenga kutathmini mafanikio, changamoto na mikakati ya sekta ya uchukuzi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
#TCAA
#usafiriwaanga
TCAA imeshiriki Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi (JTSR), uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Novemba 16, 2026, jijini Mwanza.
Ujumbe wa TCAA umeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Bi. Mtumwa Ameir.
#TCAA #usafiriwaanga
Happy International Air Traffic Safety Electronics Personnel (ATSEP) Day!
A heartfelt appreciation to all ATSEP professionals around the world — the heroes behind the scenes.
#TCAA
#usafiriwaanga
Board decisions on applications for air and ground handling services licences
For more information and full details of the Board decisions, please visit the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) official website: tcaa.go.tz.
#TCAA
TCAA YAKUTANA NA WADAU KUPITIA MAOMBI YA LESENI ZA HUDUMA ZA ANGA
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za Mamlaka katika kuimarisha ushirikishwaji wa wadau, uwazi na uzingatiaji wa taratibu katika utoaji wa leseni za huduma za usafiri wa anga.
#TCAA
#usafiriwaanga
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekutana na wadau wa sekta ya usafiri wa anga katika kikao cha kusikiliza maoni ya umma kuhusu maombi ya leseni za utoaji wa huduma za usafiri wa anga nchini, Novemba 11, 2026, Makao Makuu, Banana, Dar es Salaam
#TCAA
#usafiriwaanga
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri Bakari, amepokea ujumbe wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Malawi ukiongozwa na Bw. Alfred Mtilatila, tarehe 9 Novemba 2026, Dar es Salaam. Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika sekta ya usafiri wa anga.
Statement by Dr. Jabiri K. Bakari, Director General of the Tanzania Civil Aviation Authority, at the Seventh ICAO Worldwide Air Transport Conference, Montréal, Canada. #TCAA #ICAO #usafiriwaanga
Statement by Hon. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (MP), Minister for Transport, at the Seventh ICAO Worldwide Air Transport Conference, Montréal, Canada.
#TCAA #ICAO #usafiriwaanga
Wataalamu wa usafiri wa anga kutoka nchi 48 za Afrika wamemuenzi marehemu Peter Erasto Chinyama wa TCAA kwa dakika moja ya ukimya katika kikao cha AASPG, Zambia.
Marehemu alichangia kuimarisha usalama wa anga na kutoa mafunzo kwa wataalamu zaidi ya 150 barani Afrika.
Tanzia
#TCAA #usafiriwaanga
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri Bakari, amepokea ujumbe kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Singapore ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa, Bi. Alberenee Sim, tarehe 3 Novemba 2026, Dar es Salaam.
#TCAA #usafiriwaanga


























