Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, anatarajiwa kuongoza maelfu ya Watanzania katika maombi maalumu ya kitaifa yatakayofanyika Novemba 20, 2026, City Park, Mbeya, kwa ajili ya kuliombea Taifa amani, umoja, upendo na mshikamano. Zaidi ya washiriki 500 wamethibitisha kushiriki.
Nimeona taarifa zikisambaa mitandaoni kwamba MV Mwanza imegonga mwamba asubuhi ya leo. 😳
Kuna nini hasa kimetokea? Tatizo ni nini? Wenzetu mliopo Mwanza, tunaomba mtupe taarifa zaidi kuhusu tukio hili.
Inasikitisha sana!
Angel Wariael Noel (13) aliyejeruhiwa kwa risasi kwenye uti wa mgongo wakati wa vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Alikuwa na ndoto ya kupona na kuwa daktari, lakini amefariki kabla hajazitimizia.
Hauwezi kugombana na baba mkwe halafu ukapatane na mtoto wako ukasema nimepatana na baba mkwe!
Kupatana na kundi moja hakumaanishi umetatua mgogoro na kundi jingine. Kila mgogoro unahitaji kushughulikiwa na wahusika wake.
Kuna tofauti kati ya kupatana na mtu na kutatua mgogoro.
Matokeo ya chaguzi zisizo huru na za haki zinazopelekea akili ndogo zilizojificha katika kivuli cha uongozi kutawala akili kubwa!
Hii ndio sababu ya hitaji la Katiba Mpya itakayopelekea upatikani wa Tume Huru ya Uchaguzi na "yenye meno" itakayosimamia "Uchaguzi huru na wa Haki"
Povu lote la UVCCM ni kwa sababu hawataki kuambiwa ukweli kuhusu matendo yao, au wanataka hata wale waliojifunza mbinu chafu za rushwa kutoka kwao wawajibishwe?
Mende hawezi kuangusha kabati, Badala ya kumshambulia anayeibua kero, ni vyema UVCCM wajibu tuhuma kwa hoja!





