mobappdev retweeted
Leo umetimia mwaka mmoja tangu mauaji yaliyofanywa kwa makusudi na vyombo vya dola vya Tanzania dhidi ya Watanzania wasio na hatia.
Mauaji ya October 2025 yalikua yanaweza kuepukika na uchaguzi ukafanyika kwa amani na usalama.
Kwasababu ya kiburi na uchu wa madaraka watawala waliamua kupuuza wito wa mda mrefu wa viongozi wa dini, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na hata watu maarufu ya kutaka mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki.
Mpaka sasa mwaka mmoja baadae Nchi iko kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa, watu wanaendelea kutekwa, kuuawawa na kupotezwa.
Kila anaetoa sauti ya kukemea uovu na kutaka maridhiano na uwajibikaji wa kweli anakabiliwa na kifo au mashitaka ya uongo.
Inaonekana hawa watawala wameshindwa kujifunza kwa yale mabaya yaliyotokea, Inaonekana wanafurahia kuendeleza utawala wa mkono wa chuma, udikteta na ubabe, mauaji, utekaji na kunyamazisha badala ya kushawishi na kutatua matatizo.
Kwa kutumia njia hizi mbele ni giza tupu, hakuna sehemu ambayo utawala wa kibabe Umefanikiwa kunyamazisha watu wote, Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 70, hakuna siku watu wote hawa watanyamazishwa kwa uongo na kikundi kidogo cha watu kwa kutumia ubabe.
Njia pekee ya kutatua mkwamo huu ni.
1. Kumuachia Mwenyekiti Lissu na kufuta kesi za uongo dhidi ya wanachama wetu wote.
2. Kuachia mateka wote na kusitisha utekaji na mauaji ya kiholela.
3. Kuruhusu msuluhishi huru (mediator) kuleta watu pamoja na kuzungumza kwa ukweli na uwazi.
4.Uwajibikaji bila upendeleo kwa wahusika wa mauaji, kulipa fidia familia za wahanga, kutibu majeruhi wote na kuwapa fidia.
5. Kuruhusu Uchunguzi huru na kuomba radhi mbele ya Watanzania kwa makosa makubwa yaliyofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia wake.
6. Kuandika katiba mpya ya Nchi na sheria za uchaguzi ambazo zitarudisha umoja na haki kwa kila mtu.
7. Kutamka kwa uwazi kwamba makosa kama yale hayatajirudia tena kwenye Nchi yetu.
8. Kuhakikisha familia zinapata miili ya wapendwa wao na kufanya maziko ya heshima, kiafrika na kidini.
Kuendelea kutumia ubabe ni kuchochea chuki, uhasama na visasi kwa siku zinajazo…
Watawala badala ya kutumia chawa na ubabe kujaribu kuhujumu Chadema na uongozi wa Chadema, Tumia busara kufanya jambo sahihi la kuponya Nchi hii.
Tunajua mipango yenu dhidi yetu, lakini haki haijawahi kushindwa.
Endeleeni kupumzika kwa amani wote mliouwawa kikatili na kibabe, poleni majeruhi na wahanga wote.
Haki inaweza kuchelewa Lakini haki itapatikana tu.
mobappdev retweeted
Kutaka kuweka tozo nyingine ya barabara ni wizi wa wazi wazi. Tayari Watanzania wanalipa kodi ya barabara kila wanaponunua mafuta. Huyo aitwaye Waziri wa Ujenzi au jina lolote lile la Wizara hiyo ajue hilo. Kwa wastani Mtu Mwenye gari ya uwezo wa CC 2500 kwa mwaka analipa si chini ya shilingi milioni mbili hadi tatu za Kodi ya kutumia Barbara. Shida hapa si malipo ya fedha bali matumizi yake kwani falsafa ya waliotwaa madaraka kwa kumwaga damu ya maelfu ya Watanzania ni "kula Kwa urefu wa kba zao". Sasa hapo kutakuwepo fedha za kujenga barabara?
mobappdev retweeted
Breaking 🚨 A very dangerous attack on Netanyahu in Tel Aviv it appears he has sustained severe injuries, and an aircraft is being dispatched to transport him to the United States. This is clearly evident from the footage. Don't remove my video X Twitter
Readers added context they thought people might want to know
Claims of a dangerous attack on Netanyahu in Tel Aviv with severe injuries are false; no such event is reported by credible media, and the video shows a 2013 attack on Bulgarian politician Ahmed Dogan.
english.factcrescendo.com/2026/04/13/201…
theguardian.com/world/benjamin…
timesofisrael.com/netanyahu-desp…
srilanka.factcrescendo.com/english/no-net…
Replying to @Jambotv_
Njia ya haki ni uchaguzi huru,na nyie ccm hamtaki uchaguzi huru na haki
Replying to @Barongo01
Ameishi na baba yake msasani sana!!!huenda Joseph Kabila amezaliwa Tanzania
Replying to @bajabiri
Road Fund kwenye kila lita ya mafuta ni nini???ccm imechoka haifai watanzania
Replying to @jamiivoice
Kodi ya Tanroads ipo kwenye mafuta Road Fund😭😭😭
Replying to @Salamaenrich
Upo sahihi kabisa,baada ya lissu kumfunga na kuona zero reaction,atafuata @HecheJohn kisha eti waliobaki wakae nao meza moja😭😭😭na 2030 itakua imefika @jjmnyika @godbless_lema @Mwabuk2Boniface @ExMayorUbungo @MariaSTsehai @mangekimambi @HildaNewton21 @lifeofmshaba
Replying to @zoetjesheeftX
Upo sahihi kabisa,Ugali chakula cha wanyama
Replying to @omaryMkiza
@mshambuliaji alipiga pesa balaa.Ni dalali wa waovu 😭😭😭
mobappdev retweeted
Masisiemu yakiwa na jambo lao yanafosi kingi sana.
Huyu FREDI tangu lini alikuwa msaidizi wa LISSU? Na Djumbe atakuwa nani?
Huyu si ndio aliiba hela za LISSU mpaka familia wakaamua kumkamata? Huo usaidizi wa LISSU umeanza lini?
Changamoto kubwa iliyopo CHADEMA, tulifanikiwa kumuondoa MBOO WE ila kuna TAKATAKA zake nyingi sana kila kona ya nchi.
Uchaguzi ujao tutasafisha UPUMBAVU wote wa MBOO WE lazima tusimamishe watu tunaoongea nao lugha moja.
Unalazimisha CHAMA kiongee na masisiemu kiongee nini?
Masharti ya CHAMA kuzungumza huyu hajayasikia?
Unauza uoga kwa watu ambao tupo IMARA kuendelea na mapambano kwa manufaa ya MASISIEMU.
TAKATAKA KABISA🚮
mobappdev retweeted
MAZUNGUMZO!
Rev Peter Simon Msigwa
27/10/26
Kwa nini mtu anayejiona kuwa mhanga wa mfumo fulani anaweza kufikia hatua ya kuamini kwamba yeye ndiye anayepaswa kuomba msamaha, kujishusha na kupiga magoti mbele ya mfumo anaoulalamikia?
Hili si swali dogo. Ni swali linalohusu saikolojia ya ukandamizaji, hofu na namna watu wanavyoweza kuzoea mazingira ya kunyimwa haki kiasi cha kuanza kuona haki zao kama hisani ya wenye mamlaka.
Ninawasikia baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakisema kwamba chama kinapaswa kujishusha mbele ya watawala ili kuwe na maridhiano.
Nina swali moja: Kujishusha kwa sababu gani? Kuomba msamaha kwa kosa gani? Na kuomba huruma ili tupewe haki gani ambayo Katiba haijatambua?
Kuna tofauti kubwa kati ya kauli hizi mbili:
“Tuzungumze ili kutatua mgogoro.”
Na
“Tujishushe ili wenye mamlaka watuhurumie.”
Ya kwanza ni njia ya kutafuta suluhu yenye kuheshimiana. Ya pili inaweza ni dalili ya watu kuanza kukubali kwamba haki zao zinategemea utashi wa wenye mamlaka.
Katika saikolojia kuna dhana inayoitwa Learned Helplessness, hali ambayo mtu aliyekabiliwa na vikwazo kwa muda mrefu anaweza kuanza kuamini kwamba hana uwezo wa kubadili mazingira yake.
Badala ya kuhoji anayemnyima haki, anaanza kujihoji mwenyewe. Badala ya kudai sheria iheshimiwe, anaanza kutafuta namna ya kumfurahisha mwenye mamlaka.
Wengine wanaweza kulinganisha hali hii na Stockholm Syndrome, ingawa hiyo ni tashbihi tu, si utambuzi wa kitabibu kwa watu wenye maoni tofauti ya kisiasa.
Lakini tusichanganye mambo.
Mazungumzo si udhaifu. Maridhiano si usaliti. Na msimamo thabiti si uadui dhidi ya amani.
Swali ni: Tunafanya mazungumzo juu ya msingi gani?
Je, tunataka haki za kikatiba zitekelezwe, au tunataka kupewa ruhusa ya kuzifurahia?
Je, tunataka sheria itawale, au tunataka huruma ya watawala ichukue nafasi ya sheria?
Je, tunataka maridhiano yanayoshughulikia chanzo cha mgogoro, au maridhiano yanayofunika dalili zake na kuacha chanzo kilekile?
Haki inayotegemea huruma ya mwenye mamlaka si haki iliyohakikishwa. Ni fadhila inayoweza kuondolewa wakati wowote.
Ndiyo maana ninawauliza wenzangu wanaotaka CHADEMA iombe maridhiano:
Je, mnataka mazungumzo yatakayohakikisha haki zinalindwa, au mnataka chama kikubali masharti ya watawala ili tu kiweze kufanya siasa?
Hatuwezi kujenga taifa la haki ikiwa kila anayelalamikia kunyimwa haki anaambiwa yeye ndiye mwenye wajibu wa kujishusha kwanza.
Wajibu wa serikali si kusubiri wananchi waombe huruma. Wajibu wake ni kuheshimu Katiba, kutekeleza sheria kwa usawa na kulinda haki za wote, wakiwemo wanaoikosoa.
Tunaweza kukaa mezani bila kupiga magoti. Tunaweza kutafuta amani bila kuuza haki. Tunaweza kukubali mazungumzo bila kukubali kwamba aliyenyimwa haki ndiye mwenye hatia.
Maridhiano ya kweli hayapimwi kwa kiwango ambacho upande mmoja umejishusha, bali kwa kiwango ambacho pande zinazohusika zimekubaliana kurejesha haki, kujenga uaminifu na kuzuia makosa yasijirudie.
Tusifundishe kizazi chetu kwamba ili upate haki lazima kwanza umpendeze anayeshikilia mamlaka. Tuwafundishe kwamba mamlaka yenyewe yanapaswa kutii Katiba.
HATUHITAJI HURUMA ILI TUWE NA HAKI. TUNAHITAJI KATIBA NA SHERIA ZIHESHIMIWE.
mobappdev retweeted
Heche amtaka Ruto kusaidia kupatikana kwa Twaha Mwaipaya
bbc.in/3VXD0rh
mobappdev retweeted
Replying to @MariaSTsehai @HildaNewton21
Oh kumbe ni @godbless_lema ndiye aliyemshauri @John_Pambalu arudi Tanzania kwamba ameshaongea na Mafwele msaidizi wa Wauwaji wa ccm kwamba Pambalu atakuwa salama!
Ahsante galfriend @MariaSTsehai kwa ufafanuzi huu. Unajua mambo kama haya sio ya kuficha ficha, ni kutaja hadharani














