Pinned Tweet
Mithali 9:11
Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Amina π
Happy Birthday π To Me π
Necto Kitiga retweeted
#KENYA: UPINZANI KENYA WALAANI UTEKWAJI WA MWANAHARAKATI MWAIPAYA
Vuguvugu la Linda Mwananchi limetoa taarifa kali kulaani utekwaji wa mwanaharakati wa upinzani kutoka Tanzania, Twaha Mwaipaya, katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos, likionya kuwa Kenya inageuzwa kuwa uwanja wa kukandamiza sauti za upinzani katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa ripoti za Amnesty International, Mwaipaya alitekwa akiwa ndani ya teksi na watu waliokuwa wakitumia magari matatu. Hadi sasa hajulikani alipo.
Linda Mwananchi imetaka mamlaka za Kenya zitoe mara moja taarifa kuhusu alipo, kuhakikisha usalama wake na kuzuia kuondolewa kwa nguvu kutoka nchini.
Taarifa hiyo imeunganisha tukio hili na mfululizo wa utekaji wa mipakani, ikikumbusha kisa cha kiongozi wa upinzani wa Uganda Dkt. Kizza Besigye aliyechukuliwa Nairobi Novemba 2024 na kupelekwa Uganda, pamoja na utekwaji wa mwanaharakati wa Tanzania Maria Sarungi Tsehai Januari 2025.
Linda Mwananchi imeshutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kushindwa kulinda taswira ya Kenya kama kimbilio la wakimbizi wa kisiasa, ikionya kuwa taifa linaweza kuonekana kushirikiana na utawala kandamizi wa kikanda.
Vuguvugu hilo limeitaka kufanyike uchunguzi huru na kuwawajibisha wote waliohusika, likiahidi kuendelea kusimama kidete kulinda demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria katika ukanda huu.
Necto Kitiga retweeted
natumai kokote aliko twaha mwaipaya yuko salama. pole kwa familia, na ndugu na jamaa wote, wanaoingia kwenye kipindi kigumu. natumai hakitadumu, na twaha atapatikana. tuendelee kutahadharisha kwamba kuwinda wakosoaji, hata nje ya nchi, hakulinufaishi hili taifa. inaliangamiza!
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa wito wa kitaifa kwa makanisa yote wanachama nchini kuungana katika maombi maalum ya toba, rehema, amani na haki, kuelekea kutimiza mwaka mmoja tangu kutokea kwa matukio ya mauaji na umwagaji damu wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Wito huo umetolewa katika taarifa rasmi iliyosainiwa na Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Stanley Hotay ikielekezwa kwa Maaskofu, Viongozi Wakuu, na Wakuu wa Makanisa yote wanachama wa CCT nchini.
Katika taarifa hiyo, CCT imebainisha kuwa ni wajibu wa Kanisa kumwomba Mungu kulirehemu taifa na kuponya majeraha ya matukio yaliyopita, ili kuzuia kujirudia kwa umwagaji damu na kuvunjika kwa amani.
"Wote tunafahamu kuwa ni takribani mwaka mmoja tangu matukio ya mauaji, umwagaji damu na uvunjifu wa amani kutokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, hivyo kama Kanisa ni wajibu wetu na inafaa tumwombe Bwana, Mungu wetu; Aturehemu na kutusamehe kwa dhambi na makosa wetu kama taifa na kwa kumwaga damu isiyo na hatia katika Taifa". Imeeleza taarifa hiyo.
Dkt. Hotay ameongeza kuwa maombi hayo yanadhaniwa kuwafariji waliofiwa na kuleta uponyaji kwa waliojeruhiwa, akisisitiza"Tumwombe Mungu atulinde dhidi ya kurudia matukio kama hayo na atujalie amani, haki, umoja na maridhiano ya kweli katika Taifa letu la Tanzania".
Akinukuu Neno la Mungu kutoka 2 Mambo ya Nyakati 7:14, Dkt. Hotay ameitaka jamii kujinyenyekesha mbele ya Mungu, kuacha njia mbaya ili Mungu aisikie nchi na kuiponya.
Mbali na maombi ya amani na haki, taarifa hiyo ya CCT imegusia pia utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) unaoonesha uwezekano wa mvua kubwa na maafa, ikihimiza waumini kuomba Mungu kuepusha mafuriko, uharibifu wa mali, mazao, miundombinu, magonjwa, na kupoteza maisha.
Dr. Hotay ameeleza kuwa waumini wanapaswa kuomba ili Mungu ajaalie mvua za wastani zitakazosaidia kilimo na ustawi wa taifa, pamoja na kupewa hekima ya kuchukua tahadhari zinazostahili.
Akinukuu Maandiko Matakatifu ya Isaya 43:2 na Zaburi 46:1, Dr. Hotay amesema, "Kitabu Cha Zaburi 46:1 kinatukumbusha kuwa: 'Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.' Kwa hiyo, sisi kama Kanisa na viongozi tuendelee kumtegemea Mungu kwa imani, hata katika nyakati hizi za matetesho ya Maafa na majaribu ya amani na haki katika Taifa Letu, huku tukiendelea kutenda kwa upendo na kujenga amani katika jamii zetu".
CCT imewataka viongozi wote wa makanisa wanachama kuongoza maombi hayo katika ibada, mikutano ya maombi, na vikundi vya waumini kote nchini.
Necto Kitiga retweeted
" Kenya cannot remain the abduction hub of East Africa. Kenyan authorities MUST urgently intervene to save Twaha Mwaipaya's life and secure his safe release," Alex Mukasa, Human Rights Defender on the abduction of Twaha Mwaipaya.
#FreeTwahaMwaipaya #EndAbductionsEA #PASNet
Necto Kitiga retweeted
Twaha Mwaipaya amepotelea wapi? Heche anaitaka Kenya kuchukua hatua za haraka na kutoa taarifa kuhusu alipo mwanaharakati huyo, huku shinikizo likiongezeka kutaka ukweli ujulikane. π
bbc.in/4sq1THX
Necto Kitiga retweeted
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula leo, Oktoba 26, 2026, huku chama hicho kikieleza wasiwasi kuhusu kuzuiwa kwa mawakili wake kumwona Gerezani.
Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA, Mawakili watatu wa Lissu ambao ni Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame, walifika Gerezani leo kwa lengo la kukutana na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia.
CHADEMA imesema hali hiyo inazua wasiwasi kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa Lissu na namna haki zake zinavyolindwa akiwa gerezani, hasa wakati huu ambao ameanza mgomo wa kula.
Chama hicho kimezitaka mamlaka husika kuruhusu mawakili wake kukutana na Lissu bila vikwazo visivyo na msingi wa kisheria, huku kikisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama na ustawi wake.
CHADEMA imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mwenyekiti wake na itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya suala hilo.
#KitengeUpdates
Necto Kitiga retweeted
Tundu Lissu amejiunga na orodha ya viongozi waliotumia mgomo wa kula kama silaha ya kushinikiza madai yao. Lakini historia inasema nini kuhusu ufanisi wa njia hii?
bbc.in/4zbKPs3
Necto Kitiga retweeted
πππππππππ ππππππππππ πππ πππππππππ ππ
ππππππππ πππππππππ πππ πππππ ππππππ πππ
ππππππ ππ ππππππ ππππ
πππππππ, πππππ. ππππππ, πππππππ ππ, ππππ.
Necto Kitiga retweeted
The abduction of opposition figures and human rights defenders from the region on Kenyan soil must end. We demand that the government immediately disclose Twaha Mwaipayaβs whereabouts and ensure his safety.
πππππππππ ππππππππππ πππ πππππππππ ππ
ππππππππ πππππππππ πππ πππππ ππππππ πππ
ππππππ ππ ππππππ ππππ
πππππππ, πππππ. ππππππ, πππππππ ππ, ππππ.
Necto Kitiga retweeted
#FreeTwahaMwaipaya | STATEMENT: RISING TRANSNATIONAL REPRESSION IN EAST AFRICA SHOULD CONCERN REGIONAL JUDICIARIES AND THE INTERNATIONAL COMMUNITY
We strongly condemn the reported abduction of Twaha Mwaipaya, a Tanzanian opposition activist.
"No individual should be subjected to abduction or denied due process. Any allegations must be addressed through lawful procedures that uphold fundamental rights and the rule of law."
#ULSAT70 #ResistLawlessness
#FreeAllPoliticalPrisoners
#BangTheTable #BackOnTrack
#RNBVsion2060
@TheCitizenTz @nilepostnews @DailyMonitor @newvisionwire @TheLegalReports @TheChanzo @BBCAfrica @EACJCourt
VIDEO:
Mtandao na Muungano wa Mashirika ya Kiraia, Watetezi wa Haki za Binadamu na Wanaharakati barani Afrika (The Pan-African Solidarity Network- PASNET) umelaani vikali kile ulichokieleza kuwa ni kutekwa kwa mwanaharakati wa Tanzania na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Twaha Mwaipaya, huku ukitaka Mamlaka nchini Kenya kuchukua hatua za dharura kuokoa maisha yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 26, 2026, Mtetezi wa Haki za Binadamu, Alex Mukasa, amebainisha kuwa Mwaipaya alitekwa Oktoba 25, 2026 katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya, nchi ambayo alikuwa amekimbilia kutafuta hifadhi na usalama.
Kwa mujibu wa taarifa za PASNET na mashirika ya haki za binadamu (ikiwemo Amnesty International), Mwaipaya alitekwa majira ya asubuhi akiwa safarini kwenye teksi kwenda kuwatembelea marafiki zake, ambapo watu waliomteka walikuwa wakitumia magari matatu, likiwemo gari la aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop
βKenya haiwezi kuendelea kuwa kitovu cha utekaji katika Afrika Mashariki. Mamlaka za Kenya zinapaswa kuingilia kati kwa dharura kuokoa maisha ya Twaha na kuhakikisha anaachiwa mara moja", ameeleza Mukasa.
Mukasa ameeleza kuwa uwepo wa taarifa za mashuhuda kuhusu magari yaliyotumika ni vidokezo madhubuti vya kiupelelezi vinavyopaswa kufanyiwa kazi mara moja na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa nchini Kenya ili kubaini mahali alipo na kumpata akiwa salama.
Necto Kitiga retweeted
Mtandao wa Pan-African Solidarity Network (PASNet) umeitaka Serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais William Ruto kuhakikisha inazuia uhamisho wowote haramu wa mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Salim Mwaipaya, ambaye inadaiwa alitekwa katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya, Oktoba 25, 2026.
Katika taarifa yake iliyotolewa Oktoba 26, 2026, PASNet imesisitiza kuwa mamlaka za Kenya zinapaswa kuhakikisha Twaha anapata ulinzi na kwamba hakuna hatua ya kumhamisha kwenda Tanzania inayofanyika kinyume cha sheria.
Mtandao huo umesema Twaha aliripotiwa kutekwa akiwa ndani ya teksi, huku mashuhuda wakidai kuona magari matatu yakihusishwa na tukio hilo, yakiwemo gari aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.
PASNet pia imetaja taarifa zilizoripotiwa na mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai kuhusu madai ya mahali Twaha alipo na uwezekano wa gari kutoka Tanzania kutumwa kumpokea katika mpaka wa Tarakea.
Mtandao huo umeitaka Serikali ya Kenya kuhakikisha Twaha anapata fursa ya kuwasiliana na familia yake na mawakili wake, pamoja na kupata huduma huru za kitabibu, huku uchunguzi wa kina ukifanyika kuhusu mazingira ya kutoweka kwake.
PASNet imesisitiza kuwa mamlaka za Kenya zina wajibu wa kuhakikisha sheria zinafuatwa katika hatua zozote zinazohusu Twaha, ikiwemo kuzuia uhamisho wowote usio halali na kuwawajibisha wote watakaobainika kuhusika na ukiukwaji wa sheria.
Mtandao huo umetoa wito kwa Serikali ya Kenya, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kufuatilia suala hilo na kuhakikisha haki za Twaha zinalindwa kwa mujibu wa sheria za Kenya na wajibu wa kimataifa wa haki za binadamu.
Necto Kitiga retweeted
Tunashukuru WAKENYA wanaoungana nasisi kwenye kipindi hiki kigumu.
#FreeTwahaMwaipaya
Repost 200
Necto Kitiga retweeted
Wahuni wamemuotea Homeboy wanguπ
Haya mambo yanaumiza sana, tumekua tukiyakemea kwa miaka sasa.
Hatutaacha, hatutachoka kuendelea kuyakemea.
Unapoona matukio kama haya usiache kukemea, nitakwambia kwanini!!
Hili genge la watekaji halitumiki kuteka tu wapinzani, wanaharakati wanaoikosoa serikali na wanaojihusisha na siasa NO.
Ni genge hili hili hutumika na litatumika kuteka, kupoteza na kuua watu kwa sababu za kimahusiano, biashara na mambo mengine kwa maslahi ya watu fulani.
Usiamini, usipuuze, usifurahie na kujiona uko salama kwa sababu tu hujihusishi na siasa au hukosoi watawala na serikaliβ¦.
NO BODY IS SAFE MY DEAR.
Ipo siku utaingia kwenye 18 zao either kimahusiano, kibiashara, kinamna yoyote ileβ¦.na utapitia mateso haya haya wanayopitia wanaharakati!!
Huu sio utamaduni wa kuu~entertain au kuukalia kimya utaendelea kuota mizizi hadi kizazi kijacho!!
Tuungane kwa pamoja kuupinga!!
Twahaβ¦β¦.it hurts to look at your pictures without knowing where you are or what youβre going through.
I pray for your safety and may the blood of Jesus protect you.
We want to hear your voice and see you smile again.
Come home safely home boy β€οΈ
Necto Kitiga retweeted
The @LindaMwananchi_ statement on the abduction of Tanzanian activist Twaha Mwaipaya .

































