TzConnect retweeted
Kabudi aagiza watumishi waachie majengo ya kupanga, waende Mtumba mwananchi.co.tz/mw/habari/ki…
TzConnect retweeted
Memorial books in honour of the late Dr. Paul Mugambi are available at the ABH Reception and LC Block for the @UniversityEmbu community to sign and share condolences.
May his soul rest in eternal peace.
#UniversityOfEmbu #UoEm
TzConnect retweeted
Fellow Ugandans , the endorsement exercise for our next leader, Gen. @mkainerugaba, for the 2031–2036 presidency is ongoing across various districts in Uganda. Don’t be left behind! The future is now—let your voice be heard as we shape Uganda’s future together.
@PLUsecretariat #Uganda2031 @HonTwallafadil @HenryBasaliza1
TzConnect retweeted
PRESIDENT MNANGAGWA URGES IMPLEMENTATION OF ZIMBABWE-RUSSIA AGREEMENTS
President Dr Emmerson Mnangagwa has challenged Zimbabwean and Russian institutions to translate cooperation agreements into practical projects that improve citizens’ lives. He was speaking in Moscow after the signing of a cooperation agreement with the Autonomous Non-Profit Organisation for the Development of International Cooperation, following engagements with four Russian institutions on the sidelines of the third Russia-Africa Summit.
📷: Presidential Photographer John Manzongo
Source: @ZBCNewsonline
TzConnect retweeted
#HABARI Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ali Gugu, leo Oktoba 27, 2026, wamesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano inayolenga kuimarisha huduma za msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu magerezani.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega, amesema makubaliano hayo yataimarisha uratibu wa huduma hizo. Amesisitiza umuhimu wa kuweka mpango kazi na kutumia mifumo ya kidijitali kusimamia taarifa za mashauri.
Ulega amesema wafungwa na mahabusu wana haki ya kupata msaada wa kisheria bila kujali hali zao za kiuchumi. Ameeleza kuwa taasisi husika zina wajibu wa kuhakikisha huduma hizo zinapatikana magerezani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema makubaliano hayo yatawasaidia wafungwa na mahabusu kuelewa haki zao, taratibu za kisheria na hatua za kuchukua katika mashauri yao.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Jeremiah Yoram Katungu, amesema wafungwa na mahabusu 19,511 katika mikoa saba wamenufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Ameongeza kuwa watumishi zaidi ya 290 wamepatiwa mafunzo, huku Ulega na Katambi wakizindua mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa madawati ya msaada wa kisheria magerezani.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
TzConnect retweeted
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Rais wa Kenya 🇰🇪 William Ruto ameonya viongozi wa kisiasa wasiende kwenye mikutano ya hadhara wakiwa wamelewa na kusema maneno yasiyoeleweka.
Akizungumza Jumapili, Septemba 27, 2026, katika ibada ya kanisani huko Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta, Rais Ruto alisema:
“Huwezi kuwa kiongozi kisha uende mkutano wa hadhara ukiwa umelewa, halafu uwaambie watoto wasilewe.”
Aliongeza kuwa uchaguzi ulifanyika miaka minne iliyopita, lakini baadhi ya viongozi wanaendelea kuzungumzia mada hiyo “kwa sababu ya kuchanganyikiwa.”
Rais Ruto hakumtaja Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa jina. Hata hivyo, maoni hayo yamefasiriwa na vyombo vya habari kama majibu ya kwa kauli za Uhuru zilizotolewa siku chache zilizopita, ambapo alidai aliamini marehemu Raila Odinga alishinda uchaguzi wa 2022.
#MeaMswahiliUPDATES
TzConnect retweeted
💧 Maji unayokunywa ni salama kweli?
Hata maji yaliyo salama kwenye chanzo yanaweza kuchafuliwa wakati wa kuchota, kusafirisha au kuhifadhi.
Kwa mujibu wa @WorldBank, watu bilioni 2.1 duniani bado hawana huduma ya maji safi na salama.
Angalia nchi yako:
data360.worldbank.org/en/atl…
TzConnect retweeted
Rais wa Marekani, Donald Trump, amekosoa mfumo wa uchaguzi nchini Brazil huku akidai kuwa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi katika baadhi ya maeneo nchini Marekani kunatoa mwanya wa kuchezewa kwa matokeo.
Trump alitoa kauli hiyo Oktoba 4, 2026, baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Brazil, ambapo matokeo yalikuwa yakihesabiwa na kutangazwa ndani ya muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alilinganisha kasi ya kuhesabiwa kwa kura nchini Brazil na hali ya baadhi ya maeneo nchini Marekani, yakiwemo Detroit, Philadelphia na California, ambako matokeo yanaweza kuchukua siku kadhaa au wiki kukamilika.
Trump alidai kuwa ucheleweshaji huo nchini Marekani unatoa nafasi ya kuchezewa kwa matokeo, akitumia kauli kali kukosoa mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo. Hata hivyo, hakutoa ushahidi unaothibitisha madai yake kwamba matokeo ya uchaguzi nchini Brazil yalikuwa yamechezewa.
#KitengeUpdates
TzConnect retweeted
YOUTH EMPOWERMENT SYMPOSIUM, TURNING YOUNG PEOPLE’S POTENTIAL INTO JOBS, BUSINESSES AND NATIONAL DEVELOPMENT
Thousands of young people are expected to converge in Harare from 4 to 5 November 2026 for the Youth Empowerment Symposium, an important platform for advancing skills development, entrepreneurship, innovation and youth participation in Zimbabwe’s economic transformation. The event which was organized by the Ministry of Youth Empowerment, Development and Vocational Training, comes at a critical juncture as Zimbabwe pursues the objectives of the National Development Strategy 2 (NDS2) and Vision 2030. Its significance lies in connecting young people with practical opportunities, strengthening their participation in national development and building the human capital required to achieve an empowered, prosperous and upper-middle-income society. The symposium also comes ahead of the 2026 YouthConnekt Africa Summit in Rwanda, where Zimbabwe is competing with Zambia to host the 2027 edition.
TzConnect retweeted
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi akisalimiana na kumfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura kufuatia kifo cha baba yake mzazi, marehemu Deusdedit Mwita Wambura, aliyefariki tarehe 24 Oktoba 2026.
Makamu wa Rais ametoa salamu hizo za pole alipoitembelea familia ya Mzee Deusdedit Wambura katika makazi ya IGP Camillus Wambura, Masaki Jijini Dar es Salaam.
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, amewataka Watanzania na wabunge kusimama imara bila hofu wala uoga na kutokubali watu wachache wasiotakia mema taifa kuandika historia ya nchi, huku akisisitiza wajibu wa kumlinda na kumtia moyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia uongozi wake uliowesha dunia kuiamini Tanzania.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo na kumshika mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Nape ameeleza kuwa uongozi bora unadhihirika pale ambapo kiongozi anakabiliana na changamoto bila kukata tamaa na kuwavusha wananchi salama. Amebainisha kuwa imani iliyooneshwa na dunia kuileta mikutano mikubwa nchini inatokana na ujasiri na uongozi wa Rais Samia wa kuivusha nchi kwenye milima na mabonde.
Vilevile, Nape ametoa wito kwa Watanzania na wabunge kuendelea kuwa wamoja na kulinda mambo makubwa ambayo nchi inapaswa kujivunia, badala ya kuruhusu nia ovu za watu wachache ziharibu historia na mwelekeo wa taifa.
TzConnect retweeted
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Jeshi la Magereza nchini Tanzania limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula kuanzia Oktoba 26, 2026.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa Oktoba 27, 2026 na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza, imeelezwa kuwa mahabusu Tundu Lissu yupo salama na hayupo katika mgomo wa kula kama ilivyoripotiwa.
Taarifa hiyo ilisambazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, ambaye pia alidai kuwa mawakili watatu wa Lissu walizuiwa kuingia gerezani. Jeshi limekanusha madai hayo na kusema si ya kweli.
Kuhusu ziara za mawakili, Jeshi limeeleza kuwa wanaendelea kuruhusiwa kuonana na mteja wao kwa mujibu wa taratibu baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake halisi, kama sheria na taratibu zinavyoelekeza.
“Taarifa hizo si za kweli na zinatakiwa zipuuzwe kwani ni za upotoshaji na zenye kuleta taharuki katika jamii,” imesema taarifa ya Jeshi la Magereza.
#MeaMswahiliUPDATES
TzConnect retweeted
📍 PANGANI, TANGA
Ujenzi wa Daraja la Pangani umefikia asilimia 72.
Daraja hilo litapunguza utegemezi wa vivuko, kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, kupunguza gharama za usafiri na kuchochea biashara pamoja na utalii katika Tanga na maeneo jirani.
TzConnect retweeted
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura, nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Oktoba, 2026, kufuatia kufiwa na Baba yake mzazi Deusdedit Mwita Wambura....
TzConnect retweeted
Wananchi, Young Africans SC wamepata ushindi wa kwanza baada ya mechi tatu za Ligi kuu ya soka ya NBC Tanzania bara wakiilaza Mashujaa FC 2-1 katika uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Wananchi wamesogea mpaka alama mbili nyuma ya vinara, Simba SC wenye mchezo mkononi, wakifikisha alama 22 baada ya mechi 9 za Ligi Kuu bara.
FT: Yanga SC 2-1 Mashujaa FC
⚽ 21' Shalulile
⚽ 76' Mzize
⚽ 07' Ngushi
#KitengeSports
TzConnect retweeted
#HABARI Dalili za awali zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wapiga kura wamejitokeza katika uchaguzi nchini Israel, huku vijana wengi wakishiriki kupiga kura, kwa mujibu wa Yossi Mekelberg, mshauri mwandamizi wa Mpango wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa taasisi ya Chatham House.
Mekelberg, ambaye kwa sasa yuko nchini Israel, amesema matokeo ya awali ya maoni ya wapiga kura baada ya kupiga kura (exit polls) yatatolewa vituo vya kupigia kura vitakapofungwa. Hata hivyo, amesisitiza kuwa mchakato halisi wa kupima maoni ya wananchi unaendelea kupitia upigaji kura.
Akizungumzia Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Mekelberg amesema idadi kubwa ya wapiga kura inaweza kuashiria kile alichokiita uchovu wa wananchi dhidi ya Netanyahu, hali inayoweza kuelekeza kura kwa vyama vya mrengo wa kushoto au vile vilivyo upande wa kulia zaidi kisiasa kuliko chama cha waziri mkuu huyo.
Mekelberg ameeleza kuwa uchaguzi huo ni miongoni mwa chaguzi zenye umuhimu mkubwa nchini Israel katika kipindi cha hivi karibuni, kutokana na athari zake zinazoweza kujitokeza katika mwelekeo wa kisiasa na uongozi wa nchi hiyo.
Ameongeza kuwa uchaguzi huo unatoa fursa kwa Israel kurekebisha na kuimarisha uhusiano wake na mataifa mengine duniani, ambao umekuwa sehemu ya mijadala inayohusiana na sera za serikali na hali ya kikanda.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
















































