mwayoli retweeted
Bill Gates alisema hawezi kuruhusu binti yake aolewe na maskini.
Miaka ya nyuma iliyopita Bill Gates akiwa tajiri namba moja duniani alihudhuria kwenye Investment and Finance Conference akaulizwa;
"Wewe ni mtu tajiri zaidi duniani je unaweza kuruhusu binti yako aolewe na masikini?"
Billy akajibu "Kwanza utambue utajiri siyo kuwa na account inayopokea na kutoa pesa nyingi, utajiri ni zaidi ya uwezo wa kutengeneza utajiri.
Kwa mfano mtu alieshinda bahati nasibu au kamari huyo wala siyo tajiri, huyo ni mtu masikini mwenye pesa nyingi.
Asilimia 90 ya millionaire walioshinda bahati nasibu baada ya miaka mitano wanakua maskini tena"
mwayoli retweeted
Baada ya miaka 8 kupita, hatimaye Daladala za Mbezi- Kariakoo kupitia Morogogoro Road zimerejeshwa tena. Daladala hizi zilisitishwa mwaka 2016 baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi kuanza ila LATRA imeamua kurejesha tena daladala hizi. Una mtazamo gani kuhusu jambo hili?
mwayoli retweeted
Rais wa korea kaskazini akikagua kiwanda cha MRLS.Alafu tunadanganywa dprk ni maskini wa kutupwa wakati sie kiwanda cha baiskeli tu ishu.
#BilaGanzi
mwayoli retweeted
Mzee wangu Stephen Wasira naomba mimi wa Canada niseme kidogo juu ya upotoshaji wenu. Kwanza kabisa nakuomba usiwalishe UJINGA hao watoto watakuja kuelimika kisha wakurushie mawe.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuua hizi nchi na mamlaka zake. Ikiwa hili ni uwongo kwa nini hamuandai mjadala wa wazi mukaja na mkataba wa muungano ili sisi tunaoambiwa tunaleta chokochoko mutusute hadharani? 😂😂😂
Falme za kiarabu (United Arab Emirate) ni muungano wa nchi saba (7) lakini nchi zote hazijapoteza majina wala utambulisho wao.
1 Abu Dhabi
2 Sharjah
3 Ras Al khaimah
4 Ajman
5 Dubai
6 Umm Al Quwain
7 Fujairah
Nchi saba hizo kila moja ina serikali yake na utambulisho wake zote zinajisimamia zenyewe kwenye mambo ambayo hayapo kwenye makubaliano ya muungano wao. Hata passport zao zimeainisha huyu ni Raia wa Emirate kutoka nchi fulani. Kwa hiyo, ujinga ambao munaueneza kwa vitisho musidhani utawasaidia katika nyakati hizi mnazidi kujifedhehesha tu.
Mkataba wa makubaliano ya muungano umeunda shirikisho la Serikali tatu (3) ya Zanzibar, ya Tanganyika na ya Shirikicho unasemaje tuna nchi moja? Ujinga huu umetoka wapi?
Tanganyika na Zanzibar zimeungana kupitia HATI YA MAKUBALIANO YA MUUNGANO (Mkataba wa muungano), ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO NI KUMI NA MOJA TU (11). Tanganyika nchi nzima ina mambo kumi na moja tu? Zanzibar nchi ina mambo kumi na moja tu?
Leteni mkataba wa muungano mufedheheke.
mwayoli retweeted
Simba Sports Club ina vyanzo vipi vya mapato? Na ina matumizi kiasi gani kwa mwaka? Watu waliolemaa akili na ama wenye ‘mentality’ za kitumwa (slave mentality) ama za kimaskini (poverty mentality), ama waliobweteka na wasiotaka kutumikisha hisia, bongo zao ana viwiliwili vyao, ama wale waliochaguaga kutumia hisia, akili na viwiliwili vya wanaume wenzao, huwaza kusifia wenye hela kama miungu watu!
Hawa hawajiamini wao na wala hawawezi kuamini wenzao kwa sababu wamegubikwa na umbumbumbu na umazwazwa wa kupindukia. Kimsingi, huu ni ugonjwa mkali wa akili uliozama kwenye hisia, bongo na viwiliwili vya waafrika. Kwamba, Kuna watu wanaweza mambo mazuri na makubwa, siyo sisi! Kwamba, hatuwezi kufanya chochote. Wengine huabudu matajiri na wala siyo ukweli, uhalisia na maarifa! Wao wenyewe wameanza kwa kujishusha na kujidharau kwenye nafsi zao, wala hawahitaji kukandamizwa ama kufungwa minyororo.
Minyororo ipo kwenye hisia na bongo zao, na wala siyo kwenye viwiliwili.
Akija mzungu na makaratasi anataka kuchimba madini ama kufunga mitambo ya kuzalisha umeme, ataaminiwa na kupewa vibali vyote faster, kisha ataenda kwao kusaka pesa, lakini akija Hamisi Kipilipili mwenye nia, uwezo, maarifa na makaratasi kama yule Mzungu, hayatosomwa na pengine makaratasi yake yasipochomwa moto basi yatatumika kufungashia vitumbua!
Ndiyo maana utajiri wa Afrika ulitawaliwa na wageni kwa miaka dahari, sababu sisi kwa sisi hatuaminiani, hatupendani na tumeshindwa kujikubali! Walianza warumi miaka 2000 iliyopita, wakaja waarabu, wazungu nk.
Naendelea kutafuta details za mapato na matumizi ya timu za Simba na Yanga, ili tuweze kufanya tafakuri tunduizi kwa pamoja, maana menejimenti yake siyo ‘rocket science’ ya kusema ni ngumu sana kueleweka; kimsingi ni hesabu rahisi tu za kujumlisha na kutoa. Kwa nchi ya watu wa mpira kama Tanzania, hivi timu kama Simba ndiyo ya kuuzwa 20bn na kutawaliwa na janja janja aliyeshindwa kulipa hiyo hela kwa kipindi cha miaka 7?
Umbile la mfanano wa hesabu (sijapata rasmi bado) za vyanzo vya mapato ya Yanga, na matumizi yake, ni hizi hapa. Naamini haziwezi kuwa na tofauti kubwa sana na za Simba. Zitazame, kama kuna makosa saidia kurekebisha, ama kama unazijua za Simba tupe tuone, kisha tutafakari pamoja!
MAPATO (YANGA):
1. SportPesa - 3bn kwa mwaka
2. Azam - 3bn kwa mwaka
3. Gate collection - 2bn
4. CAF (robo fainali) - $900,000 (Kama TZS - 2.4bn
5. Jezi - Mkataba wa GSM Jezi 1.5bn
6. Haier - 1bn
7. Kadi za uanachama - 1.5bn
8. Ushindi Azam Federation- 500mn
9. Ongeza na mengine ambayo sijaweza kuyakadiria!
10. NBC Bank ?
JUMLA TAKRIBAN 15bn.
MATUMIZI (YANGA):
1. Mishahara (Wage bill) - 400mn/mwezi (kwa mwaka ni kama 4.8bn)
2. Makazi - 720mn
3. Kodi - inaweza kuwa 3bn
4. Unaweza kutuongezea matumizi mengine ambayo unakisia yapo!
JUMLA TAKRIBAN 8.5bn.
My take:
1. Inafikirisha sana hisa 49% za Simba kuuzwa 20bn tu
2. Inafikirisha sana kusikia ‘mwekezaji’ hewa anasema anapata hasara
3. Inafikirisha sana ‘mwekezaji’ hewa kushindwa kulipia hizo hisa zake mpaka leo (takriban miaka 7!)
4. Inafikirisha sana Menejimenti ya Simba kushindwa kusajili wachezaji wazuri zaidi na kuwalipa vizuri wachezaji wetu wawe na motisha uwanjani
5. Inafikirisha sana timu zetu kukosa hata kambi zake za kudumu za maana, gymnasium na spa zake za kisasa, viwanja vyake, makazi ya kudumu n.k.
TIBA:
1. Mifumo ya governance iboreshwe
2. Ukiweka mfumo mzuri wa governance(utawala), utapata Menejimenti nzuri, na Menejimenti itasimamiwa ipasavyo.
3. Ukiweka mfumo mzuri wa governance utapata uwazi (transparency) wa mapato na matumizi.
INAWEZEKANA!
#HK #Fighter #NjeYaBox #NguvuMoja #DaimaMbeleNyumaMwiko
mwayoli retweeted
Thousands of people being killed weekly,mostly women & children who also get enslaved for labour to extract Cobalt in Congo 🇨🇩 for US and Chinese Companies to make Electronic Products. 💔😭
mwayoli retweeted
KITABU CHA HENOKO
SEHEMU YA PILI.
Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4: 22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.
BASI..... Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza
Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.
Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.
Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.
CATHOLIC THEOLOGICAL REFLECTION.
Wanateolojia Wakanisa Husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa (MWANZO 3: 15) kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.
Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.
👍👍👍
mwayoli retweeted
KITABU CHA HENOKO (THE BOOK OF ENOCH)
SEHEMU YA KWANZA
- Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko.
Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na Baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa Babu wa Nuhu (MWANZO 5: 21-23).
Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni (YOSHUA BIN SIRA 44 :16) (WAEBRANIA 11:5). Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.
TUANZE....
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki La Magharibi(Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi wa uhakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashariki la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana, Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa (2SAMWELI 1: 18) Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri..... (Ngoja Tuendelee)
BASI...... Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa kupingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.
Ukisoma Kitabu cha (HENOKO 6:1-8) ni sawa na Ukisoma (MWANZO 6:1-8) lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya (YUDA 1:6) Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri (MWANZO 6:2) Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)
Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.
Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika (MWANZO 6:2-4) Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao.
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).
Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7: 11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao. 📝📝📝
mwayoli retweeted
Elimu ya chuo kikuu ni muhimu lakini karama ya kutunza pesa na kuzalisha pesa ni muhimu kuliko elimu ya chuo kikuu cha sasa.
Ndio maana wenye pesa ambao hawana Elimu wanatafuta Elimu ya chuo kikuu na wenye elimu ya chuo kikuu wanatafuta pesa.
Msomi wa shahada ya Uchumi,ananunua simu ya Tsh 2,500,000/= baada ya kumaliza chuo anamuomba mzazi mtaji wa Tsh 3,000,000/= Najiuliza Mwanaume Shoga anayesomea Sheria ana akili au Elimu?
Binti anayeuza mwili wake na anasomea shahada Psychology,ana elimu au akili .? Elimu yetu ya sasa vyuo vinatafuta wanafunzi na sio wanafunzi kutafuta vyuo.
Naona Elimu yetu haina tija kwa sasa yajitajika mabadiliko sababu sio sifa njema kupoteza miaka 4 chuo kikuu na kukaa mtaani miaka 5.
The purpose of the university is to make students safe for ideas – not ideas safe for students.
mwayoli retweeted
Mnapenda sana kujua historia ya maisha yangu eti? 😀 I will tell you something, it is interesting; you know why? It was never smooth. Chapeni kazi ili mje kuwa na cha kuhadithia uzeeni.
NB:- Nilimaanisha kuwa nilifanya internship Muhimbili miezi 11 na wiki 6 (za rotation ya mwisho). Sawa na kusema miezi 11 na wiki 2.
Wakati tunafanya mgomo wa mwisho enzi zile, mwaka 2005 December, nilikuwa namalizia rotation yangu ya mwisho kule Obs & Gyn, Nilikuwa wiki ya 6, Bado wiki mbili nimalize internship.
Tupofukuzwa kufuatia mgomo, tulikaa mtaani. Tukasota sana. Story for another day!
Tuliporudishwa mimi nilipangiwa kwenda kurudia rotation yangu ya mwisho pale Mwananyamala; miezi miwili (wiki 8!).
Binafsi nilipanga kwenda kufanya kazi wilayani mbali kabisa na jiji baada Ya hapo, hivyo niliamua kujitolea pale Mwananyamala, kwenye idara za surgery na obs&gyn ili kujifunza upasuaji!
Nilifundishwa kazi sana na Madaktari wa pale, mmojawapo nilikuwa naye karibu sana alikuwa Dr. Kapinga, yuko huko kwenye mipira mipira huko siku hizi. Huyu alitupokea kwa mikono miwili maana wengi walikuwa wanatuogopa na kutunyanyapaa vijana tuliotoka kwenye mgomo! 😀
Baada ya hapo nilipewa ajira Hospitali ya Rufaa ya Kitete, Tabora. Nakumbuka Mhe. Dr. Tizeba alikuwa DC Sikonge na alitamani kunivuta wilayani kwake, na ndiye alinipambania sana niende kule baada ya kupokelewa Kitete. Bahati mbaya Kitete sikupokelewa vizuri, sababu ya historia ya migomo. Hapa nilichukia sasa na kuachana na ajira ya serikali mpaka nilipokuwa Mbunge.
Replying to @kenanmalindisa
Mbn hesabu rahisi tuu, intern unaweza ukafanya ata miezi 18 .
Kuna kuongezewa week ujue kwa makosa ya kinidhamu au kitaaluma apo ndugu @HKigwangalla huenda aliongezewa week au alichukua likizo
#Njeyabox 😁






























